RAIS MWINYI AFUNGUA MKUTANO MZITO WA WANAHISA WA CRDB ARUSHA , AAHIDI MAZINGIRA WEZESHI YA UWEKEZAJI TAASISI ZA FEDHA ZANZIBAR

Na Joseph Ngilisho Arusha


Rais wa Zanzibar na Mwenyekitiwa wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema serikali yake itaendelea kuweka mazingira rafiki ya uwekexaji  katika sekta za kifedha ili kuleta tija kwaajili ya kukuza uchumi wa nchi hiyo.

Akizungumza Jijini Arusha Mapema leo May 17,2024 katika Semina maalumu iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kuelekea katika Mkutano wa 2 wa wanahisa unao endelea katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC.

Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa katika kukuza uchumi hapa nchini kunahitaji mazingira bora kwa wawekezaji hasa katika sekta ya fedha maana fedha ndiyo kitovu cha ukuaji wa uchumi kokote duniani.

"Niwashukuru sana Benki ya CRDB kwa kuanzisha programu mahususi Zanzibar kitu ambacho kwa sasa kinaimarisha uchumi wetu na niwahaidi kuendelea kushirikiana nanyi wakati wote kwa ustawi wa nchi yetu". Ameeleza Dkt. Mwinyi.

Aidha pia katika upande wa ukuaji kiuchumi Dkt. Mwinyi amesema kupitia sekta ya utalii hivi sasa wawekezaji wameanza kujenga hoteli katika visiwa na fukwe mbalimbali Zanzibar na kuwataka wanahisa wanapo pata gawio kuendelea kuwekeza ndani ya Benki hiyo kwa maslahi mapana ya uchumi.






"Niwaombe wanahisa kuendelea kuwekeza hisa ndani ya benki ya CRDB pindi mnapo pata gawio na kuzifanyia kazi vyema ili kuleta chachu zaidi katika kukuza uchumi pamoja na kuimarisha ushirikiano na serikali dhidi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa letu". Ameeleza Dkt Mwinyi.

Aidha pia Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa kupitia programu ya benki hiyo ya CRDB, ukuaji wa uchumi,sekta ya michezo programu ya Inuka na uchumi wa kigitali umesaidia kukuza uchumi wa bluu ikiwemo makongamano ya wadau wa sekta ya kilimo katika kuongeza tija.

"Uwekezaji wa CRDB na utendaji imara wa watumishi umekuwa ni mnyororo muhimu katika kuhakikikisha benki inatoa mchango kupitia faida kutoka kwa wanachama na kutoa mchango kwa serikali kwenye miradi ya maendeleo na kurithisha jamii kwa vitendo kwa kuimarisha muungano wetu wa miaka 60 kwa vitendo". Amesisitiza Dkt. Mwinyi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, ameeleza kuwa mafanikio tunayoyaona, leo kwa Benki yetu yanatokana na utashi wa kisiasa, mazingira mazuri ya kibiashara ambayo yamewekwa na serikali zetu, ya Muungano, pamoja na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na ushirikiano wa kimkakati ambao tumekuwa nao.

"Benki yetu imeendelea kuwa na ukuaji endelevu mwaka hadi mwaka. Taarifa ya Mwaka wa Fedha 2023 inaonyesha Benki yetu imepata Faida Baada ya Kodi ya Shilingi Bilioni 423 ikiwa ni ongezeko la asilimia 21 kulinganisha na mwaka 2022,huku tukishuhudia ukuaji mkubwa katika". Amesema Nsekela 

"Vilevile ameeleza kuwa ukuaji huu tunaendelea kuushuhudia hata mwaka huu ambapo matokeo ya robo ya kwanza ya mwaka yanaonyesha Benki imepata Faida Baada ya Kodi ya Shilingi Bilioni 128 kulinganisha na Shilingi Bilioni 90 iliyorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana 2023". Ameongeza Nsekela.

Matokeo haya ya ukuaji wa faida ni kiashiria cha ukuaji wa pamoja kwa utendaji wa Benki, kukua kwa thamani ya uwekezaji wa wanahisa,pamoja na kuboresha maisha ya wateja na jamii kwa ujumla kupitia uwezeshaji na uwekezaji unaofanywa na Benki yetu na kampuni zake tanzu". Amesisitiza Nsekela

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Hussein Laay amemweleza Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rasmi kuwa Bodi ya Wakurugenzi imependekeza nyongeza ya asilimia 11 kwa gawio kwa hisa ambayo itapelekea gawio kuwa Shilingi 50 kwa hisa kutoka Shilingi 45 kwa hisa.

"Hii ni kutokana na ufanisi wa utendaji wetu unaopelekea ukuaji wa thamani ya uwekezaji wa Wanahisa wetu". Ameeleza Laay.

Dkt. Laay amesema ukuaji huo wa gawio unakwenda unawanufaisha Watanzania wengi, kwani asilimia 80 ya umiliki wa Benki ni Watanzania pamoja na Serikali.

Aidha Mwenyekiti huyo wa Bodi ameendelea kwa kuelezea kuwa umiliki huo pia umegusa pande zote mbili za Muungano kwani umiliki wa Serikali zetu kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii unahusisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ambao wanamiliki hisa zaidi ya Milioni 41 ambazo ni takribani asilimia 1.6 za hisa

Mwenyekiti wa Bodi ameendelea kwa kuelezea kuwa umiliki huo pia umegusa pande zote mbili za Muungano kwani umiliki wa Serikali zetu kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii unahusisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ambao wanamiliki hisa zaidi ya Milioni 41 ambazo ni takribani asilimia 1.6 za hisa zote za Benki ya CRDB.

Ameeleza kuwa 46 .l 34% Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita uwekezaji wa ZSSF umekuwa ukiongezeka ukiakisi mafanikio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi Mhe. Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.









3nds


Post a Comment

0 Comments