MKURUGENZI HALMASHAURI AIVULIA KOFIA TUMAINI SENIOR SEKONDARI, ATAKA SHULE ZA SERIKALI ZIKAJIFUNZE MBINU ZA UFAULU,

 Na Joseph Ngilisho ,MONDULI 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli ,Happiness Laizer amesema  ,katika halmashauri  yake,shule binafsi na za mashirika ndiyo zinazofanya vizuri kitaaluma na kuzitaka shule za serikali kuiga mbinu zinazotumiwa na shule hizo ili kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri zaidi kimasomo.


Laizer ametoa Kauli hiyo jana wakati alipohudhulia mahafali ya 3 ya kidato cha sita katika shule binafsi ya Tumaini Senior sekondari iliyopo Makuyuni wilayani Monduli Mkoa wa Arusha na kuipongeza shule hiyo kwa kuwa kinara wa ufaulu na hivyo kuiwakilisha vema kitaaluma halmashauri hiyo.

"Shule binafsi na zile za mashirika zina nafasi kubwa katika ufaulu katika halmashauri yetu utakuta katika matokeo ya kidato cha nne ama cha sita zimefaulisha kwa asilimia 100 na mimi niwapongeze kwa kusimamia vizuri taaluma hiyo ninachoshauri  shule za serikali zitembelee ili kuchukua mbinu zinazotumiwa na shule binafsi"

Alisema ubora wa shule ya Tumaini Senior sekondari kwa miaka mitatu umekuwa juu sana na alizitaka  shule zingine kuiga mfano huo ili kuwapatie elimu bora wanafunzi hasa wanaotoka katika jamii ya kifugaji.

Aidha Mkurugenzi huyo aliwapongeza wanafunzi 53 waliohitimu masomo yao alidai wameshinda vishawishi ambavyo vingeweza kuharibu ndoto yao ya masomo na kuwaomba wazazi kuwalinda watoto hao  ili wakaendelee na masomo ya juu.

Awali Mkurugenzi wa shule ya sekondati Tumaini Senior, Modesty Bayo alisema kuwa mafanikio ya shule yake yanatokana na namna wanavyosimamia taaluma kwa kuzingatia mitaala mbalimbali iliyopo pamoja na mitaala yao waliojiwekea shuleni hapo.

Alisema shule yake inazingatia sana masomo ya sayansi yanayotokana na mitaala ya wizara ya elimu nchini,pia shule hiyo  imejiongezea mitaala ya ziada inayoitwa stemp program  Science Technology engineering end Mathematics) inayowasaidia vijana kufanya utafiti na kufanyiakazi tafiti hizo  katika kumjenga mwanafunzi kutatua changamoto zake akiwa shuleni ama nyumbani.

Alisema elimu hiyo ya stamp inafundishwa shuleni hapo  kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita pia alisema wanatoa elimu ya kujitegemea inayohusu kilimo na ufugaji  ambayo inamjenga Mwanafunzi kuwa na ujuzi utakaomsaidia kujiajiri popote aendako baada ya kuhitimu masomo yake.

Akiongelea suala la Malezi alisema shule yake imefanikiwa kwa kiwango cha juu kuwa na malezi bora watoto katika maadili mema na wanauhakika huko waendako watakuwa kioo kwa wenzao.

Mkuu wa shule hiyo Sifael Msengi alisema jumla ya wanafunzi wapatao 53 wamehitimu masomo yao na kutunukiwa vyeti na kwamba taratibu wa kupokea wanafunzi wengine wa kidato cha tano zinaendelea na kuwakaribisha wazazi kuendelea kuleta watoto wao ili wapate malezi na elimu bora.








Ends...
















Post a Comment

0 Comments