MFANYABIASHARA AANGUA KILIO AKIIDAI HALMASHAURI YA MONDULI MILIONI 227,KWA MUDA WA MIAKA 18,NI BAADA YA KUKAMILISHA UJENZI SHULE YA SOKOINE

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Mfanyabiashara na mkazi wa jiji la Arusha, Patrick Swai ameangua kilio mbele ya mkuu wa Mkoa wa Arusha,Paulo Makonda akilalamikia halmashauri ya Monduli kushindwa kumlipa madai yake ya  sh, milioni 227.7 yaliyodumu kwa takribani miaka 18 baada ya kukamilisha ujenzi wa shule.


Akiongea na vyombo vya habari alisema kuwa aliingia makubaliano na halmashauri hiyo kwa nyakati tofauti ,kujenga shule ya sekondari ya Ole Sokoine iliyopo kata ya Monduli juu katika halmashauri hiyo ,pamoja na kusambaza vifaa vya ijenzi .

Alisema katika mikataba walioingia na halmashauri hiyo yenye thamani ya sh,milioni 456.1, mwaka 2007 ilikuwa ni pamoja na kujenga Madarasa ,Mabweli na nyumba za walimu.


Alisema 2013 waliingia makubaliano mengine ya ujenzi  Maabara ,Nyumba ya Mkuu wa shule ,Matundu ya vyoo , matenki ya Maji na kukarabati sehemu ya jengo hilo.



Katika kipindi chote cha makubalino  halmashauri hiyo iliweza kumlipa kiasi cha sh,milioni 228.3 tu na kubaki deni la sh, milioni 227.7 ambalo hadi sasa bado anasotea hajaweza kulipwa na kupelekea mfanyabiashara hiyo kuishi maisha ya taabu.


"Wakati wa ujenzi wa mradi huo nilikopa fedha benki  kwa ajili ya kukamilisha mradi huo baada ya kuombwa  na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo hayati Edward Lowasa aliyekuwa ameambatana na Laigwanani wa Eneo hilo Meijo Ole Kisongo"


Alisema kutokana na kuchelewa kwa malipo hayo  nyumba yangu ya biashara pamoja na mitambo yangu ya ujenzi iliuzwa  na benki ili kufidoa deni alilokuwa akidaiwa  baada ya kushindwa kulipa mkopo  kutokana na kucheleweshwa kwa madai yake.


Aliongeza kuwa katika ujenzi wa mradi huo alipoteza gari lake moja baada ya kudumbukia korongoni kwenye kina kirefu wakati akipakia mchanga na mawe kutoka umbali mrefu.


Akiongea kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na mkuu wa mkoa Paulo Makonda wilayani humo, alimweleza jinsi halmashauri hiyo imeshindwa kumlipa fedha zake hatua ambayo imesababisha aishi maisha ya kubangaiza.


Alisema licha ya malalamiko yake kuyapeleka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ,na katibu tawala David Lyamongi kuiandikia barua halmashauri hiyo mwaka 2020 ya kuitaka imlipe madsi yake mfanyabiashara huyo mwenye kampuni ya ujenzi ya God's enterprise co ltd,lakini bado aliendelea kupigwa danadana na watawala wa halmashauri hiyo.


Swai alimweleza mkuu huyo jinsi anavyopata tabu katika kuendesha maisha yake kwani ameshajaribu kila njia ya kupata msaada wa madai yake lakini amekuwa akiambukia patupu.


Katika Mkutano huo Makonda alimhoji  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Happiness Laizer juu ya madai hayo iwapo anamfahamu mlalamikaji pamoja na madai yake.


Mkurugenzi alijibu kuwa deni hilo halipo kwenye kumbukumbu za halmashauri hiyo na yeye alipata kusikia madai hayo katika juma la haki katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha  lililoendeshwa na mkuu huyo wa Mkoa kwa wanancho kutoa malalamiko na kero zao.


Hata hivyo Makonda aliendelea kumng'ang'ania Mkurugenzi huyo kwa kumwamuru kumlipa mfanyabiashara huyo kwakuwa anatambua shule hizo za kata zilijengwa na mfanyabiashara huyo aliyekuwa akisambaza vifaa vya ujenzi.



"Mheshimiwa mkuu wa mkoa kwa sasa halmashauri haina fedha ila kuna fedha zetu tunatarajia kulipwa na Shirika la umeme Tanesco "alisema Mkurugenzi huyo.


Swai ameiomba serikali kumsaidia kupata fedha zake kwani kipindi hicho alitumia rasilimali zake zote baada ya uongozi wa halmashauri hiyo kumwomba kuwajenga shule hizo za kata baada ya rais wa kipindi hicho Jakaya Kikwete kuagiza ujenzi wa shule za sekondari kata pamoja na maabara.

Ends...










Post a Comment

0 Comments