NAIBU GAVANA BOT ASISITIZA MATUMIZI YA KIDIGITALI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIFEDHA YATACHOCHEA MAENDELEO

Na Joseph Ngilisho ARUSHA  


Naibu Gavana wa Benki Kuu Tanzania (Bot) ,dkt Yamungu Kayandabila amesema  matumizi ya kidigitali katika utoaji wa  huduma za kifedha , yatachangia  maendeleo endelevu katika soko la kifedha na hivyo kurahisisha utoaji wa  taarifa  sahihi na kwa wakati.


Dkt Kayandabila amesema hayo jijini Arusha wakati alipokuwa akifungua semina ya siku tatu iliyoandaliwa na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu (NBAA) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).


Alisema ubunifu wa mabadiliko  ya kidigitali utarahisisha taarifa  za kifedha kupatikana kwa wakati na kwa uwazi zaidi,taasisi zinazofanyakazi na kuziwezesha  kupatikana kwa huduma za uwazi na ufanisi kwa wateja wao.


"Faida za mabadiliko ya kidigitali ni uwezo  wa kutoa huduma za kifedha ambazo hazijafikiwa kuendesha ushirikishwaji wa fedha kwa kupanua benki ya simu  na nyingine za kidigitali na bidhaa zinazostawi"








Alisema kuwa ujio wa mabadiliko hayo ya kidigitali kunahitaji uwekezaji mkubwa katika miundo mbinu ya teknolojia, ubireshaji endelevu wa nguvu kazu hatua za usalama wa mtandao.


"Tunapoanza njia hii ni muhimu tubaki tukizingatia hitaji la ukuaji jumuishi na endelevu na dhamira ya kujenga thamani kwa wadau wote pamoja na wafanyabiashara"


Awali Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania (NBAA),CPA Pius Maneno,alisema mkutano huo wenye washiriki zaidi ya 700 kutoka sekta mbalimbali za umma na binafsi nchini, watajadili mada mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya kidigitali katika utoaji wa huduma za kifedha na taarifa za kifedha.


Pia watajadili mada ndogo ndogo 11 ambazo zitalenga kuangalia wakaguzi wa ndani kuhusu masuala ya kidigitali pamoja na kuangalia miongozo mbalimbali iliyopo.Majukumu ya wahasibu ,wakaguzi na mabenker katika utambuzi wa fedha haramu.


Mada nyingine itahusisha maendeleo endelevu kwa kutumia digitali katika masoko ya hisa ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi ,changamoto za matumizi ya kidigitali, masuala uwekezaji endelevu na utoaji wa taarifa, pia matumizi ya kidigitali katika brela ili kuendeleza makampuni nchini.


Ends....









Post a Comment

0 Comments