MAONYESHO YA KARIBU KILIFAIR KUTIKISA ARUSHA WANUNUZI ZAIDI YA 600 DUNIA KUTUA ARUSHA,KAMPUNI YA MEDIA WORKS YAJIPANGA KWA MACHAPISHO YA BIDHAA ZA KITALII

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA

WANUNUZI  zaidi ya 600 wa Utalii kutoka nchi  40 duniani , waonyeshaji  na wadau 468 wa utalii kutoka nchi 37,  wamethibitisha kushiriki maonyesho ya kimataifa ya Karibu -Kilifair  yanayotarajia kuanza Juni 7 hadi 9 mwaka huu katika viwanja vya Magereza jijini Arusha.


Wadau hao na wanunuzi  wa  utalii  watapata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii, ili kujionea vivutio vilivyopo ,wakawe mabalozi wazuri kwenye nchi zao.




Akizungumza jana jijini Arusha Mkurugenzi wa Kilifair Ltd ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo Dominic Shoo alisema lengo la maonyesho hayo ni kutangaza vivutio vilivyopo ndani ya nchi  na kuvitangaza nje ya nchi kupitia wageni wa maonesho hayo.


"Siku hizi tatu tunatarajia kuwa na kiwango kikubwa cha biashra kwa sababu lengo letu kubwa  kukutanisha wadau toka mataifa mbalimbali duniani, kuja kujua vivutio vyetu hapa Tanzania, wavitembelee na kuweza kuwa mabalozi wazuri, kwa ajili ya kuuza vivutio vya Tanzania,"alisema.


Alisema mwaka huu onyesho hilo ni kubwa kuliko la mwaka jana, sababu  wamekua na waonyeshaji zaidi na mwamko wa  wanunuzi ni mkubwa kuliko mwaka jana na wamekua na kiwango cha juu, kuliko mwaka jana kutokana na vitu ambavyo wameweza kuvinunua, ili kuhakikisha onyesho hilo linalingana na hadhi ya viwango vya kimataifa.


Aidha alisema pia Juni   8  watakuwa na tamasha la muziki, utakaoleta watu pamoja na utakuwa wa kiwango cha kimataifa kutokana na kushirikisha wataalamu wa burudani.


"Kwa  sababu siku hizi tatu tumeona tutakuwa na wageni wengi Arusha, lakini hawana burudani ya kutosha tukaona  kuliko  wakapate burudani sehemu tofauti, ambazo hazina hadhi tumeamua kuwaandalia kitu kipya kitakachowapa burudani Juni nane mwaka huu,hapa hapa viwanja vya Magereza  na tumeunga na wataalamu wa burudani tunashirikiana nao,"alisema.


Hata hivyo alisema utalii unakua, ambapo  msimu huu wa utalii umefunguka mapema ukilinganisha na mwaka jana, ina maana huhitaji wa kiu ya kwenda kwenye hifadhi  ni mkubwa.


"Lakini   watu wana hoteli mpya nyingi na wanabishara mpya, wanataka kuhakikisha wengi wanazijua na kupitia hapo wajue taarifa zao na bei zake,"alisema


Kwa mujibu wa Shoo, maisha sasa hivi ni Afrika, ukienda nje ya nchi  onyesho lolote linalokosa Mtanzania wanashtuka, sababu Afrika mkombozi wao  Tanzania kwenye sekta ya utalii.


Aliyataja baadhi ya mataifa hayo yafakayoshiriki knyesho hilo, kati ya 40 wanakotoka wanunuzi wa utalii kuwa ni  Ujerumani, Amerika, Italia, nchi za Afrika Mashariki, Afrika Kusini na  Asia. 


Maonyesho hayo yanatarajia kufunguliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki.


Daniel Sambai kutoka Serena Hoteli alisema  kila mwaka kumekuwa na ongezeko la wanunuzi, hali hiyo  inatokana na uongozi na usimamizi imara  wa waandaji wa onyesho hilo.


Mkuu wa kitengo  cha masoko na mauzo,  kutoka kampuni ya Media Works, Noel Petro aliiomba serikali kuruhusu ujenzi wa  mabanda ya maonyesho ya kudumu, ili kuwepo kwa mazingira salama nyakati zote, badala ya kusubiri wakati wa onyesho tu.



"Kutokana na maonyesho haya,ni ya kipekee kwetu sisi, yanaleta fursa ya utalii kwani wateja wetu wakubwa zaidi ya asilimia 70  wanatokana na utalii."alisema.

Akiongelea huduma  zao wanazotarajia kuzitoka katika maonyesho hayo alisema wamejipanga kuja na punguzo  la aina yake katika uchapishaji wa  bidhaa zabkitalii zikiwemo nguo aina ya  t-shirt pia wamekuja na pidhaa mpya za chupa za maji ambazo ni rafiki wa mazingira

Ends.....


Post a Comment

0 Comments