JIJI LA ARUSHA LAANZA KUTEKELEZA KWA KISHINDO MRADI WA TACTIC ,LAPOKEA MAGARI MAZITO MAZITO NA KUYAKABIDHI KWA MHANDISI, GAMBO ASEMA MRADI UTAJIBU KILIO CHA WANANCHI

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Ln
Halmashauri ya jiji la Arusha, imekabidhi Magari mawili kwa Mhandisi  wa jiji hilo kwa ajili ya shughuli za miradi ya uendelezaji Miji wa TACTIC inayotekelezwa katika jiji hilo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami katika kata mbalimbali za jiji hilo.

Magari hayo ambayo yamenunuliwa na serikali ya Rais Samia yatakuwa mali ya halmashauri hiyo na kwamba Mkurugenzi wa jiji hilo Mhandisi Jumaa Hamsin aliyakabidhi kwa Mhandisi wa jiji hilo.

Akikabidhi magari hayo jana Mhandisi Hamsin alitoa rai kwamba yatumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa kwa lengo la kuharakisha mradi huo ili kuwaondolea changamoto wananchi wa jiji hilo.

"Katika  mradi wa TACTIC wenye ufadhili wa benki ya dunia, jumla ya Magari manne yametolewa na serikali ila yaliyokabidhiwa leo ni Mawili na mengine yapo njiani yanakuja"

Alisisitiza kuwa Nyenzo hizo ni muhimu sana wakati wa kutekelez mradi huo kwa ajili ya kurahisisha shughuli za mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kuharakisha  maendeleo ya wananchi na kwamba jiji la Arusha kupitia mapato yake ya ndani limenunua magari 8 likiwemo basi dogo .

"Leo tumeongeza vitendea kazi kwa ajili ya mradi wetu wa TACTIC, tumekabidhi magari mawili kwa mhandisi wa jiji kati ya magari manne ya mradi huu, lakini sisi kama halmashauri tumenunua pikapu sita,Landcruser moja na basi dogo  moja.

Awali mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo alisema kuwa mradi wa TACTIC ni mradi unaoenda kujibu kero kubwa za wananchi kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami ikiwemo barabara ya Engoshelatoni, Olasiti na Oljoro.

Alisema mradi huo pia utatekelez ujenzi wa soko la kisasa la Kilombero na Morombo ,ujenzi wa kituo cha kisasa cha  mabasi .

Sisi wananchi wa Arusha tunamshukuru sana rais Samia Suluhu Hasani kwa kutupatia mradi huu pamoja na vitendea kazi vya magari manne ambapo leo magari mawili tumemkabidhi mhandisi kwa ajili ya kurahisisha shughuli za ujenzi wa miundo mbinu hiyo"

Ends...









Post a Comment

0 Comments