Gambo, DC wararuana mbele ya RC Makonda, nusura wazichape ..usinichokonoe
Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Paulo wa Makonda amejikuta kwenye wakati Mgumu kushindwa kuamua nani mkweli kati ya Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa na Mbunge wa Arusha Mrisho Gambo wakati wakipeana mipasho kwenye mkutano wa hadhara.
Alianza mkuu wa wilaya ya Arusha,Felisician Mtahengerwa wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi katika wilaya yake ,kwa kumweleza RC Makonda jinsi mbunge huyo alivyo tatizo katika wilaya yake kwa kukwamisha shughuli za maendeleo.
Mtahengerwa pamoja na mambo mengine alimweleza namna Mbunge Gambo anavyokwamisha shughuli za maendeleo ikiwemo kutokuwa na maelewano na watendaji wa halmashauri pamoja na kwenda kinyume na maamuzi ya baraza la madiwani.
"Mimi kama kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia halmashauri kwa upande wangu nimewaeleza kwenye halmashauri Ila Kumekuwepo na mabishano ya wazi kabisa Kati ya menejimenti , baraza la madiwani na mbunge"
"Kwa hiyo mkuu wa mkoa Malumbano, Migongano na kutoelewana baina Yao kumesababisha tuwaadhibu wananchi wetu bure ambao hawana hatia wakati serikali imeshatoa fedha Ila inapokuja kwenye matumizi inakuwa changamoto"Alisema DC
Naye mbunge wa Arusha MrishoGambo akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa RC MAKONDA katika viwanja vya Kilombero alipewa nafasi ya kusalimia wananchi ndipo alipotumia nafasi hiyo kujibu mapigo .
Alimweleza RC Makonda kwamba DC ameshindwa kuwasimamia watendaji ipasavyo ndio maana hawazingatii majukumu yao na kumwambia asimchokonoe jambo lililomkasirisha DC nakuonekana akimkazia macho na kunyosheea kidole.
Gambo pasipo kujali aliendelea kumnanga kwa kusema ...
"DC asinilazimishe kugombana nawe,mimi nimetulia,tufanye maendeleo, tufanyekazi acha chokochoko"
RC Makonda alisema kwa kifupi 'waacheni hawa wanajuana kwa viremba' .
0 Comments