BENKI YA CRDB YAMKABIDHI RC MAKONDA PIKIPIKI 20 ZA ULINZI ,MAKONDA AMTAHADHALISHA RPC IWAPO UHALIFU UTAENDELEA,POLISI WASUBIRI AHADI YAKE YA BAISKELI 100 ,PIKIPIKI 30 NA MAGARI 20

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


Benki ya CRDB imekabidhi pikipiki 20 zenye thamani ya sh,milioni 150 kwa mkoa wa Arusha kwa lengo la  kuimarisha usalama  katika mji huo wa kitalii.


Akiongelea tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, AbdulMajid Nsekela alisema msaada huo umekuja kupitia mpango  wa benki hiyo wa kutenga asilimia 1 ya faida inayoipata kila mwala kwa ajili la  kurejesha kwa jamii kupitia sekta ya elimu,Afya .

Alisema kila mwaka benki hiyo imekuwa ikifanya ukutano ukitanguliwa na mkutano wa wanahisa ambao huenda sanjari na kushiriki shughuli za kijamii ikiwemo kukabidhi Madawati ujenzi wa madawati ikiwa ni mpango wa kuunga mkono juhudi za Raisi Samia Suluhu.

"Leo hii tupo Arusha kufanya mkutano wetu wa 29 pia  tutafanya makabidhiano ya pikipiki 20 kwa mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuimarisha usalama na kukuza sekta ya utalii ikiwa ni kuunga mkono  jitihada za Rais wetu katika sekta ya utalii"

Aidha Nsekela alielezea jinsi Benki hiyo ya CRDB inavyokuwa mstari wa mbele kupitia sera yetu ya Uwekezaji kwenye Jamii na kumhakikishia kuwa uwekezaji huu unaolenga kwenye sekta ya Afya, Mazingira, Elimu, Vijana na Wanawake unafanyika nchi nzima ikiwa ni sehemu ya mchango wa Benki ya CRDB katika ustwai wa jamii inayotuzunguka.

Hafla hiyo ya makabidhiano ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mkoa wa Arusha, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, pamoja na Wakurugenzi wa Bodi ya Benki yetu, na baadhi ya viongozi wa Benki ya CRDB.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika hoteli ya Gran Melia ambapo Nsekela alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paulo Makonda ambaye naye alimkabidhi kamanda wa polisi Mkoani Hapa, Justine Masejo .

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ambaye ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuunga mkono adhma ya mkoa huo ya kuhakikisha kuwa usalama upo wakati wote ikiwa ni sehemu ya kuchagiza ukuaji wa utalii.

Makonda alisema sekta ya utalii ina umuhimu mkubwa katika uchumi na maendeleo ya wananchi nchini kwani ndiyo inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni, ikiwa ya pili kwa kuchangia kwenye Pato la Taifa, na ya tatu kwa kutoa ajira.
"Nilipokutana na makamanda wa polisi Mkoani Arusha nilitamani kuwaongezea nyezo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi ili kuwahakikishia wananchi wetu na mali zao hususani watalii wanaotembelea mji wetu wa Arusha "
"Nilitoa ahadi ya kuwatafutia vitendea kazi ,niliahidi pikipiki 50,baiskeli 100 za umeme na magari 20 nashukuru CRDB imekuwa ya kwanza kutuwezesha pikipiki 20 naamini ndani ya miezi mitatu nitatekeleza ahadi yangu ili kazi ya ulinzi tuweze kuulizana na kamanda wa polisi"

Alisisitiza kuwa nyenzo hizo walizokabidhiwa leo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuimarisha doria maeneo mbalimbali ili kuhakikisha watalii wanaotembelea Arusha wanabaki salama mpaka muda wao wa kuondoka .

Aliwaonya wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kuacha mara moja kwani jeshi la polisi lipo macho na watashughulikiwa kikamilifu.

Naye kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justine  Masejo aliishukuru benki hiyo ya CRDB kwa msaada huo akidai kuwa wapo macho kuhakikisha wanalinda raia na mali zao usoku na mchana ikiwemo watalii wanaotembelea Mji wa Arusha.









Ends..







Post a Comment

0 Comments