Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Baraza la uongozi la Taasisi ya Kiislam ya Twarika , limemwomba mkuu wa mkoa wa Arusha, Paulo Makonda kushirikiana na taasisi zote za dini mkoani hapa bila kubagua na kuepuka taarifa chonganishi,majungu na fitina ambazo akiziendekeza zitafanya ashindwe kufikia malengo ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Msemaji mkuu wa Twarika Taifa,Sheikh Haruna Husein, wakati wa hafla fupi ya kutangaza viongozi wapya wanaounda baraza la uongozi , iliyofanyika katika msikiti mkuu wa Zawiya uliopo Matejoo, Makao nakuu ya Twarika jijini Arusha.
Sheikh Haruna alimwalika mkuu huyo wa Mkoa kufika katika taasisi hiyo aweze kuombewa na kupata baraka za viongozi hao wa dini ili aweze kusimama imara katika uongozi wake akiwa na hofu ya mungu hasa kipindi hiki taifa linapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa.
"Sisi viongozi wa dini tunawajibu wa kukaa karibu na serikali yetu pamoja na viongozi wote wanaochaguliwa na kuteuliwa, katika kuwajenga kiimani ili taifa letu liendelee kubaki na imani "
Aidha aliwataka viongozi wanaochanguliwa kukubali kuachia madaraka pindi muda wao unapofika kwa kupokezana vijiti na hiyo ndio desturi yetu watanzania jambo ambalo litasaidia kuondoa mifarakano na machafuko yasiyo na tija katika nchi yetu.
Awali mwenyekiti wa Twarika Taifa,Ally Rashird aliwaomba viongozi wa dini nchini,kushikamana na kushirikiana vema na serikali katika kudumisha amani iliyopo ili wananchi waweze kunufaika na uongozi wao na taifa liendelee kubaki salama.
"Sisi viongozi dini na serikali lazima tuwe kitu kimoja ,tuoneshe mshikamano na upendo kwa watu wote '
Awali akitangaza baraza hilo katibu mkuu wa Taasisi ya Twarika Taifa,Abdi Omari,alisema taasisi ya Twarika ambayo ipo chini ya Baraza la waslamu Bakwata, iliingia hapa nchini mwaka 1932 na kupata usajili mwaka 2010 na imetapakaa hapa nchini na katika nchi za Afrika mashariki nanmakao yake makuu yakiwa hapa Arusha.
Miongoni mwa viongozi wanaounda baraza hilo la uongozi ni pamoja na mhimili wa taasisi ya Twarika,Sheikh Salimu Daruweshi Mti Mkavu na makamu wake, Khalifa Mbaraka Salimu.
Naye mwenyekiti wa wanawake Twarika Taifa,Rehema Athumani na mwenyekiti wa Twarika Mkoa(wanawake),Mwanaidi Hamis ,walimwomba rais Samia Suluhu kuunga mkono jitihada zao za kusaidia watoto yatima wanazozifanya kupitia misikiti mbalimbali katika maeneo ya mijini na vijijini mkoani hapa.
Ends...
0 Comments