Na Joseph Ngilisho,Monduli
Aidha mkuu huyo wa wilaya amesema ufaulu katika shule 15 za serikali zilizopo wilayani humo bado hauridhishi na kuwataka viongozi wote wa elimu wilayani humk, kuhakikisha wanapindua meza ili shule za sekondari za serikali zifanye vizuri zaidi kielimu.
Alisema Rais Samia Hassan Suluhu anatoa fedha nyingi kwaajili ya ujenzi wa shule lakini baadhi ya watoto haswa jamii za kifugaji hawapelekwi shule badala yake kwenda kuchunga mifugo jambo ambalo linafifisha elimu wilayani humo.
Alisema shule yake ya Tumaini Senior ni moja ya shule zilizofanya vizuri kwa ufaulu katika wilaya hiyo, ambapo wanafunzi wake 12 waliongoza kwa kupata division I ya 7 na kupatiwa motisha ya zawadi mbalimbali ikiwemo vyeti ,fedha na Kombe.
"Pia tuna walimu 10 wakiongozwa na mkuu wetu wa shule ambao wamefanya vizuri sana katika masomo yao na kupatia zawadi na vyeti ,huu ni mwanzo mzuri na tunatarajia kufanya vizuri zaidi na kuendelea kuwa vinara kiwilaya ,mkoa na Kitaifa "
Alisema siri ya mafanikio ni ushirikiano kati ya walimu na wanafunzi na tunatoa masomo ya kuwajenga wanafunzi wetu kujitegemea hasa katika masuala ya taaluma na mazingira pia wanafunzi wetu wanajifunza masomo zaidi ya sayansi ya kujitegemea nje ya darasa .
Kwa upande wake Mkuu wa sekondari ya Tumaini Senior, Sifael Msengi alisema shule yake imeongoza masomo 9 kati ya 10 na kushika nafasi ya kwanza kiwilaya kwa shule zote 26 za sekondari.
"Tumeongoza kwa wanafunzi 12 kufanya vizuri kimasomo kupata nafasi ya kwanza, pia tumekuwa shule bora na kupata zawadi ya ngao na vyeti ni jambo la kumshukuru mungu na tunaahidi kufanya vizuri zaidi "
Naye Kaimu Ofisa Elimu Sekondari Wilayani Monduli,Magreth Muro aliwashukuru walimu kwa kufundisha vema wanafunzi ikiwemo kuongeza ufaulu wa asilimia zaidi ya 98 na kufuta ziro kwa baadhi ya masomo ambayo wanafunzi hawajafanya vizuri
"Tunashukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule na ujenzi wa shule kilichobaki sasa walimu ni kufundisha kwa bidii ili kuongeza ufaulu kwa watoto wetu,lakini pia kuzingatia maadili na weledi"
Naye Ofisa Elimu Mkoa wa Arusha,Abel Mtupwa aliwaasa walimu kuzingatia maadili sanjari na kuepuka mikopo isiyo na tija ili kuhakikisha ufaulu unaongezeka kwani mikopo hupelekea baadhi ya walimu kupata mawazo na kushindwa kufundisha vema wanafunzi.
Pia aliwaasa walimu wa sekondari kutumia lugha ya Kiingereza kama SEHEMU ya mawasiliano zaidi na wanafunzi wao Hatua itakayosaidia kuongeza umakini kwa wanafunzi kwa kuwa masomo mengi yapo kwa lugha hiyo ."Walimu wajiepushe na tamaa ya ngono na kujihusisha na mikopo isiyo na tija ,wanakopa sana hadi hawakopesheki ,hii inashusha hadhi ya taaluma ya elimu,chukueni tahadhali ,acganeni na ulevi kudanga ba msiwe waoga wa kuongea kiingereza shuleni ndio hadi ya sekondari"
"Sisi walimu baadhi yetu tumekosa maadili wapo walimu wanaojiingiza kwenye ulevi,ukahaba kwa kuvaa nguo zisizofaa shuleni na kujihusisha na mapenzi na wanafunzi hii sio sawa lazima tufuate maadili ya kazi yetu"alisisitiza Ntupwa.
Enda....
0 Comments