TANROADS ARUSHA YAPOKEA BILIONI 2,KUTENGENEZA BARABARA ZOTE ZILIZOHARIBIWA NA MVUA,MTENDAJI MKUU TANROADS ATUA ARUSHA AJIONEA ATHARI KIBAO ATAJA MIKOA KIBAO ILIYOHARIBIWA TAZAMA HAPA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Wakala wa barabara nchini, Tanroads ,imeanza kuzifanyia matengenezo barabara zote zilizoathiriwa na mvua  zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo Mkoa wa Arusha.


Akiongea na vyombo vya habari Mkoani hapa,baada ya kutembelea kipande cha kilometa nne katika barabara ya Arusha bypass iliyoharibiwa na mvua hizo, Mtendaji Mkuu wa Tanroads Nchini,mhandisi Mohamed Besta alisema serikali imetoa kiasi cha sh,bilioni 66 kwa ajili ya matengenezo hayo katika mikoa mbalimbali nchini.

Alisema kupitia mpango wa Dharura ,mkoa wa Arusha umepatiwa kiasi cha sh,bilioni 2.2 huku akiitaja  mikoa mingine iliyokumwa na kadhia hiyo nchini ni Rukwa, Katavi, Mwanza, Kagera ,Kigoma ,Mbeya,Rufiji , Songwe na Dar es salaam.


Alifafanua  kwamba awali walifanya tathmini ya uharibifu wa miundo mbinu katika yote  nchini kwa kipindi cha mwezi januari na Februari ,ambapo hitaji la  dharura lilikuwa ni sh, bilioni 120 lakini mvua ziliendelea kunyesha na tathmini  ya mpaka sasa ni sh,bilioni 250 kwa ajili ya kurejesha barabara kupitika.


"Tunashukuru rais samia ametupatia sh,bilioni 66 na tumezisambaza katika mikoa yote iliyopata majanga ya mvua"


Aidha mhandisi besta alitoa maelekezo kwa mameneja wote wa Tanroads katika mikoa hiyo kuhakikisha wanatumia  fedha hizo vizuri ili kupunguza athari iliyojitokeza kwa wananchi na kazi hiyo imalizike kwa wakati.


Naye meneja wa Tanroads Mkoa wa Arusha, Mhandisi Reginald Massawe alisema mvua zinazoendelea kunyesha zimeleta athari kubwa katika maeneo mbalimba ikiwemo kipande cha kilometa 3.5 katika barabara ya Arusha bypass ambapo matengenezo yake yanaendelea kufanyoka usiku na mchana.


Alisema kipande hicho cha barabara kimeanza kutengelezwa kupitia kampuni ya ujenzi ya Rock Tronic LTD ya mjini Moshi kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa mawe kando ya barabara ili kuzuia mmomonyoka wa udongo.


"Mwezi wa nne tarehe  5 mvua kubwa ilinyesha na kusababisha athari kubwa kutokana na mmomonyoka wa udogo kwenye milima ya sambasha inayotokana na matumizi mabaya ya ardhi"


Alisema kazi hiyo wanatarajia ikamilike ndani ya miezi miwili na maeneo mengine yaliyopata athari ya mvua  ni pamoja na barabara ya Mbauda kwenda Losinyai, Longido ,Karatu na wanajipanga kuendelea kutembelea maeneo mengine ili kufanya tathmini ikiwemo kuzibua  makarvati yaliyoziba kwa udongo.


Kwa upande wake Mhandisi wa kampuni ya Rock Tronic Ltd inayotekeleza mradi huo wa ujenzi wa mtaro katika barabara ya mchepuo (Arusha Bypas) Mhandisi Elibahati Kihondo, ameeleza kuwa kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha wamejipanga kumaliza mradi huo kwa wakati ili wananchi wasiweze kupata athari zozote zile zinazotokana na maji yanayotoka maeneo ya milimani.


"Mpaka sasa tumeleta mashine za kutosha katika maeneo husika na tunafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kingo hizi tunazo zijenga zikamilike kwa wakati". Ameeleza Eng Kihondo.








Ends...









Post a Comment

0 Comments