Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Arusha,limewahakikishia wananchi na wakazi wa Mkoa huo kwamba hali ya upatikanaji wa nishati ya Umeme kwa sasa ni nzuri na hakutakuwepo na mgawo wa umeme tena baada ya kukamilika kwa asilimia 100 kituo chake kipya cha kupooza umeme cha Lemguru kilichopo wilaya ya Arumeru Mkoani hapa.
Akitoa taarifa hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,meneja wa Tanesco Mkoani Arusha Mhandisi, Endrew Lucas alisema hadi sasa Arusha inaziada ya umeme wa megawati 256 na hii ni baada ya kituo cha Lenguru kuzalisha megawati 225.
Alifafanua kwamba kituo chao cha kupooza umeme cha Njiro kinachopooza umeme wa kilowati 220 kutoka Babati hadi Arusha na kupeleka umeme katika Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga kilikuwa kimezidiwa ndio maana shirika liliamua kuanzisha kituo kingine cha Lemguru.
"Tuna kituo kingine wilayani Karatu kinachozalisha Megawati 16 hivyo ukijumlisha kituo cha Njiro ,Karatu na Lemguru tunakuwa na jumla ya Megawati 341 na matumizi ya yetu ya juu ya mkoa wa Arusha ni megawati 85 na hivyo tunaziada ya megawati 256"
Alisema kwa ziada hiyo ya umeme tunawakaribisha wawekezaji kwa sababu tunauwezo mkubwa wa vituo kuzalisha umeme kwa sasa.
"Kwa sasa tunachokifanya ni kujenga laini za umeme kutoka Lemguru kwa ajili ya kupunguza mzigo kituo cha Njiro na hadi kufikia leo laini mbili zimekamilika "
Akizungumzia hoja ya mkuu wa mkoa Makonda juu ya uwepo wa nguzo chafu za umeme na kuchafua jiji hilo alisema, nguzo hizo zinakuwa chafu kutokana na matumizi mseto ya baadhi ya watu wanaounganisha nyaya za mitandao ya Internet bila idhini ya shirika hilo.
Ends..
0 Comments