MPWA WA HAYATI MAGUFULI ATIWA MBARONI KWA KUSAMBAZA PICHA CHAFU ZA NGONO NA KUJIPATIA MANUFAA YA FEDHA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wawili akiwamo mpwa wa hayati John Magufuli, Furaha Dominic kwa tuhuma za kuratibu mtandao wa uhalifu wa kusambaza picha za ngono kwa lengo la kujipatia pesa.


Akizungumza na waandishi wa Habari jana Jumatatu jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum- SACP Jumanne Muliro amesema watu hao walikuwa wakisambaza picha hizo huku wakiwatisha wahusika ili kujipatia fedha.

Aliwataja watu hao ni; ‘’Furaha Dominic Jacob (32) mkazi wa Masaki na Mustapha Kihenge (28) Mkazi wa Mwenge TRA, wanatuhumiwa kutenda makosa ya uhalifu wa kimtandao. Wanadaiwa kusamba picha chafu za video za watu sizizo na maadili kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia za vitisho.

“Watuhumiwa wote wawili watafikishwa mahakamani leo Jumanne ili kukabiliana na tuhuma hizi,” alisema Muliro.

Furaha Dominic Jacob ambaye alikuwa mmoja wa makada wa CCM waliokuwa wameomba ridhaa ya chama hicho katika mbio za ubunge – Kawe kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, alishinda kura za maoni lakini akaenguliwa na Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM.

HT: Mwanahalisi 

Post a Comment

0 Comments