MFANYABIASHARA WA BAR MAARUFU YA KIPONG ARUSHA, JOHN KASIAN NA WENZAKE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KIMYA KIMYA CHINI YA ULINZI MKALI WA POLISI,ASOMEWA MASHTAKA YA UTAKATISHAJI FEDHA HARAMU,NUSURA AZIMIE MAHAKAMANI

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA

MFANYABIASHARA wa Bar Maarufu ya Kipong ya Jijini Arusha,John Kasian Shayo na wenzake wawili wamefikishwa mahakamani chini ya ulinzi Mkali wa Polisi na Kusomewa mashtaka nane likiwemo la utakatishaji fedha Haramu.

Wengine walioshtakiwa  na Mfanyabiashara huyo  ni vijana wawili  ,Issa husein Goha na Maliki Issa Mohamed wote wakazi wa mjini Arusha ambao kwa pamoja wamepelekwa gerezani mahabusu kutokana na mashtaka yao kutokuwa na dhamana kisheria.

Kasian na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo kimya kimya jioni ya leo jumanne machi 9,mwaka huu, chini ya ulinzi mkali wa polisi na baadaye kupandishwa kizimbani.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu mfawidhi Mwandamizi ,Sheila Manento wa mahakama ya wilaya Arusha, wakili wa serikali Upendo Shemkole akisaidiana na Godfrey Nugu  alisema mtuhumiwa huyo na wenzake walitenda makosa hayo kabla ya kukamatwa Machi 21 mwaka huu katika eneo la Njiro Jijini Arusha.

Alisema makosa yanayomkabili mfanyabiashara huyo  ni kutakatisha  fedha haramu sh,milioni 3.6,makosa mawili ya kughushi ,Makosa mawili ya Kughushi Nembo za biashara.

Mengine ni Makosa mawili ya kuchakachua vinywaji kwa ajili ya kuviuza na makosa mawili ya utakatishaji fedha haramu na kujipatia kiasi cha sh,milioni 3.6.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo na wamepelekwa mahabusu ya Magereza hadi Machi 23 mwaka huu watakapofikishwa tena mahakamani hapo.

Mfanyabiashara huyo alikuwa  anawakilishwa na wakili maarufu,Moses Mahuna huku washtakiwa wengine wakiwakilishwa na wakili Fridorine Bwemelo ,kesi hiyo itakuja tena mahakamani hapo Machi 22 mwaka huu.

Marchi 21 Mwaka huu majira ya usiku Kasian alikamatwa na jeshi la polisi baada ya mamlaka za serikali kuvamia eneo lake la biashara pamoja na eneo la uzalishaji na uchakachuaji wa kinywaji aina ya Konyagi.

Ends..





Post a Comment

0 Comments