Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Akitoa uamuzi huo leo mahakamani hapo,baada kupokea taarifa ya dalali wa Mahakama kutoka kampuni ya fast world kuhusu utekelezaji wa amri ya mahakama, naibu msajili wa mahakama hiyo,Mariam Mchomba alimwagiza dalali huyo kwenda kukabidhi eneo hilo kwa mshinda tuzo jambo ambalo amelitekeleza chini ya ulinzi askari polisi na viongozi wa eneo hilo.
Askofu KKAM, Philemon Mollel ,Hata hivyo wakati wa makabidhiano hayo yakifanyika Monaban alilazimika kuondoka eneo la tukio ,japo hakuridhishwa na hatua iliyofikiwa akidai hakutendewa haki.
Alan Mollel, Dalali wa MahakamaAkizungumza baada ya kukabidhi eneo hilo dalali wa mahakama ,Alan Mollel alisema amefanikiwa kukabidhi plot namba 29,30,31,32 iliyopo Ngulelo pamoja na vitu vyote vilivyokuwa kwenye ardhi hiyo likiwemo kanisa na hivyo kuibua hofu hatima ya askofu Monaban na waumini wake namna ya kusali katika kanisa hilo.
Naye wakili maarufu wa washinda tuzo Moses Mahuna alisema mgogoro wa kugombea eneo hilo umechukua muda mrefu tangia 2010 baina ya familia ya marehemu Titus aron Mollel na Philemon Mollel ila wanashukuru mahakama kwa kumaliza mgogoro huo kwa kumpa ushindi mteja wake William Titus Mollel na kufanikiwa kulirejesha katika familia ya marehemu Titus Mollel.
Alisema kwa mujibu wa sheria, mali zote zilipo chini ya ardhi hiyo zitabaki kuwa mali ya mshinda tuzo .
Kwa upande wake wakili wa Philemon Mollel, Francis Stolla alisema hakuridhika na taratibu zilizotumiwa na mahakama katika kumwondoa mteja wake katika eneo linalogombewa na kumkabidhi mshinda tuzo kwa sababu taratibu hazikufuatwa ikiwemo kutopewa nafasi ya kusikilizwa.
Alisema wamepeleka maombi mahakamani kuomba mapitio ya kesi hiyo mahakama ya rufaa ambayo yamepokelewa na wanasubiri siku ya kusikilizwa.Naye mshindwa Tuzo,Philemon Mollel alisema hakubaliani na maamuzi ya mahakama hiyo kwani imetoa upendeleo kwa upande mmoja na hivyo amewaelekeza mawakili wake kuomba mapitio ya mwenendo wa shauri hilo ili kusikilizwa upya kwa shauri hilo na kutolewa maamuzi.
Vicheko vya mawakili baada ya kuuangusha mbuyu,kushoto ni wakili Maganga na mwenzake Mahuna
Ends.....
0 Comments