MASIKINI KANISA MAARUFU ARUSHA LAVUNJWA TAZAMA VIDEO HAPA ,ASKOFU ALIA UWIII, ADAI WATAVUNA WALICHOPANDA

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Hatimaye mshinda Tuzo katika kesi ya kugombea eneo Lililopo Ngulelo jijini Arusha,William Titus Mollel ameamua kubomoa kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki KKAM, hii ni baada ya mahakama kuu kubaini kwamba umiliki wa awali wa mfanyabiashara maarufu Philemon Mollel Monaban, haukuwa kisheria na alivamia.


Kanisa hilo linalokadilia kuwa na thamani ya takribani sh,milioni 50 lilijengwa katika eneo la mgogoro na Mfanyabiashara, askofu dkt. Philemon Mollel ambaye baadaye alisimikwa kuwa askofu na  wachungaji kadhaa wa kanisa hilo walisimikwa .

Hivi karibuni waumini wa kanisa hilo walionekana kusali nyumbani kwa askofu Mollel huku baadhi yao wakiangua kilio wakidai kupokwa haki yao ya umiliki wa kanisa hilo.

Majira ya asubuhi mapema leo watu kadhaa walionekana wakivunja kanisa hilo na kung'oa mabati jambo linaloashilia  mwisho wa ndoto za waumini wa kanisa hilo kusali na kuamudu katika jengo hilo lililoanza kujipatia umaarufu mkoani hapa.

Wakati kanisa hilo likibomolewa ndani ya kanisa hilo kulikuwepo na madhabahu viti,Vitabu vya kimungu,mziki na vitambaa kadhaa ya kupamba kanisa ambavyo vyote vinabaki kuwa mali ya mshinda tuzo mahakamani.

William Mollel (Baraka)alipoulizwa juu ya kinachoendelea kanisani hapo alisema wamwamua kuvunja ili kuondoa kelele zinazoendelea juu ya kanisa hilo.

Askofu Monaban alipoulizwa juu ya hatua hiyo alisema kwa kifupi wacha wavunje na kwamba watavuna walichopanda.










Ends...



Post a Comment

0 Comments