Na Joseph Ngilisho ,ARUSHA
Hatima ya mali za mfanyabiashara maarufu na askofu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki KKAM, dkt Philemon Mollel (Monaban)Mkazi wa jijini Arusha,zilizopo katika eneo aliloamuriwa na mahakama kuondoka , likiwemo Kanisa ,itajulikana siku ya ijumaa April 12 mwaka huu wakati Mahakama ikitarajiwa kutoa uamuzi.
Miongoni mwa mali hizo ni pamoja na Kanisa ,Kituo cha mafuta matanki ya Mafuta na nyumba kadhaa zilizopo katika eneo hilo .
Jana dalali wa mahakama kutoka kampuni ya udalali ya fast world alifika katika eneo hilo lililopo Ngulelo nje kidogo ya jiji la Arusha, akiwa ameambatana na askari polisi kwa ajili ya kutekeleza amri ya mahakama kwa kulikabidhi eneo hilo kwa mshinda tuzo, ambaye ni Titus Aron Mollel.
Hata hivyo zoezi hilo halikufanikiwa baada ya mshindwa tuzo(Monaban) kupeleka maombi madogo katika mahakama hiyo ya kuiomba imruhusu aondoe malizake alizokuwa ameendeleza kabla ya kulikabidhi kwa washinda tuzo.
Akiongea katika eneo la tukio dalali wa mahakama ,Alan Mollel alisema alifika katika eneo hilo lenye ukubwa wa ekari tano kwa ajili ya kutekeleza amri ya mahakama kwa kulikabidhi kwa mshindi wa tuzo.
"Tulifika hapa kutekeleza amri ya mahakama kwa ajili ya kukabidhi eneo lililokuwa likigombewa kwa mshinda tuzo ila zoezi hilo limeshindwa kufanyika baada ya kutokea sintofahamu juu ya uhalali wa mali za mshindwa tuzo kuzichukua ama sio halali,nimepokea maelekezo ya mahakama kuwa zoezi hilo lisimame na kusifanyike kitu chochote hadi siku ya ijumaa maamuzi ya mahakama yatakapotolewa"
Wakili wa upande wa utetezi,Endrew Maganga alisema kuwa kimsingi shauri hilo namba 1 la mwaka 2017 lilimalizika mara baada ya mahakama kuu kumpa ushindi mteja wake Mei, 2021 na kutamka pasipo shaka kwamba ,Philemon Mollel alikuwa ni Mvamizi na anapaswa kuondoka.
Alisema Mollel hakuridhika na maamuzi hayo na kukata rufaa mahakama ya rufaa Tanzania chini ya majaji watatu.Februali 9 mwaka huu,mahakama hiyo ilibariki maamuzi ya mahakama kuu Arusha iliyowapa ushindi wateja wake (wasimamizi wa mirathi) wakiongozwa na Titus Aron Mollel.
Wakili Maganga alisema kuwa Aprili 5 mwaka huu mahakama hiyo ilitoa oda kupitia dalali wa mahakama iliyomteua ili Mshindwa tuzo aweze aondolewe kwa nguvu .
"Mollel ameshindwa kutii amri ya mahakama ya kuondoka kwa hiari katika eneo hilo na kulikabidhi kwa wahusika ndio maana dalali wa mahakama yupo hapa kwa ajili ya kumwondoa ila amekimbilia tena mahakamani akipigania mali zake ndio maana tumeshindwa kuendelea hadi siku ya ijumaa April 12,tutakapopata ufafanuzi wa kimahakama juu ya madai yake"alisema wakili Maganga
Naye wakili Moses Mahuna aliyekuwa akimwakilisha mshinda tuzo, alisema kwa mujibu wa sheria ya Tanzania anayemiliki ardhi anapaswa kumiliki na vitu vyote vilivyoko ndani ya ardhi hiyo hasa pale mahakama itakapobaini kuna uvamizi ulifanyika.
Alisema eneo hilo kwa sasa litakaa chini ya dalali wa mahakama kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kulikabidhi kwa washinda tuzo baada ya mshindwa tuzo kugoma kukabidhi licha ya sheria kumtaka kufanya hivyo kwa hiari.
Katika hatua nyingine wakili Mahuna alisema mteja wake amefungua kesi ya madai ya zaidi ya sh,milioni 130 akimdai gharama mshindwa tuzo(Mollel) alizotumia wakati wa uendeshaji wa kesi ya rufaa na kesi zingine nyingi alizozifungua akijitahidi kuchelewesha utekelezaji wa amri ya mahakama.
"Tumefungua kesi ya kudai gharama, tulishinda kesi kama sita alizokuwa akifungua ,tulishinda kesi Mahakama kuu ,akakata rufaa mahakama ya rufaa tukashinda,pia hakuishia hapo akafungua shauri la kuzuia utekelezaji wa hukumu mahakama kuu tukashinda,akafungua tena shauri dogo la kuongezewa muda tukashinda hivyo tumekuwa na mlolongo wa kesi nyingi"
"Siku ya Ijumaa tutakutana tena mahakamani ili mahakama impe fursa ya kusikiliza hoja zake anazojaribu kuzileta pamoja na kwamba amri ya mahakama imeshatoka na kwa mujibu wa sheria pale inapotambulika kuwa wewe ni mvamizi zile mali zitatambulika sio mali yako hivyo huna haki ya kuchukua kitu chochote ispokuwa kuondoka mara moja"
Kwa upande wake wakili wa Mshindwa tuzo,Kennedy Mapima alisema kilichotokea ni kwamba Mteja wake alitakiwa kuondolewa kwa nguvu kinyume cha utaratibu jambo ambalo alidai ni kinyume cha utaratibu wa kawaida ndio maana wameiomba mahakama iwasikilize ili taratibu ziweze kufuatwa.
"Upande wa washinda tuzo walifika mahakamani kuomba oda ya kutekeleza amri ya mahakama,lakini walipewa oda ya siku saba mteja wangu aondoe mali zake kwa amani lakini tumeshitukizwa kuona mteja wangu akiondolewa kabla ya muda aliopewa na mahakama "
"Tumeiomba mahakama isikilize maombi ya mteja wangu ikiwemo mapitio ya kesi, hivyo tarehe 12 tunatarajia kufika mahakamani kupata mwongozo wa kimahakama".
Ends..
0 Comments