By Ngilisho Tv
Mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Iran dhidi ya Israel yaliyoanza usiku wa Jumamosi tarehe 13 Aprili kwa mara nyingine tena yameibua hofu ya kuongezeka zaidi kwa mgogoro katika eneo la Mashariki ya Kati.
Ingawa hakukuwa na hasara kubwa nchini Israel, misururu ya zaidi ya vilipuzi 300 imedhihirisha uwezo wa Iran wa kushambulia kutoka mbali.
Huu ni mzozo mkubwa ambao ulikuwepo kwa muda mrefu, na mashambulizi dhidi ya Israel na makundi yanayoshirikiana na Iran, vile vile, mashambulizi dhidi ya maeneo lengwa yanayohusishwa na Iran yamechangia kuongezeka kwake.
Israel tayari iko kwenye vita huko Gaza na pia inakabiliwa na kuongezeka kwa mapigano ya kuvuka mpaka na kundi la Lebanon la Hezbollah, kwa hivyo kuongezeka zaidi kwa mapigano hayo kunaweza kusababisha hatari.
Mkuu wa majeshi ya Israel Lt Kanali Herzei Halevi amesema nchi yake itajibu mashambulizi ya Jumamosi, lakini hakufafanua zaidi.
Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Ali Bagheri Kani, ameiambia TV ya serikali kuwa shambulio la Israel litajibiwa kwa sekunde, sio masaa.
BBC imeangazia swali hili kwa kutumia vyanzo vilivyoorodheshwa hapa chini, ingawa kila nchi inaweza kuwa na uwezo mkubwa ambao haujulikani.
Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Kimkakati (IISS) inalinganisha nguvu ya silaha ya wanajeshi wa mataifa yote mawili, kwa kutumia mbinu mbalimbali rasmi na chanzo huria kutoa makadirio bora zaidi inavyoweza.
Mashirika mengine, kama vile Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, pia hufanya tathmini, lakini usahihi unaweza kutofautiana kwa nchi ambazo mara nyingi hazitoi takwimu.
IISS inasema Israel inatumia zaidi katika bajeti yake ya ulinzi kuliko Iran, ikiipa nguvu kubwa katika mzozo wowote unaoweza kutokea.
IISS inasema bajeti ya ulinzi ya Iran ilikuwa karibu $7.4bn mwaka 2022 na 2023, wakati ya Israel ilikuwa zaidi ya mara mbili ya hiyo, karibu $19bn.
Matumizi ya ulinzi ya Israel ikilinganishwa na Pato la Taifa pia ni maradufu ya Iran.
Iran ilitangaza kulichukulia shambulizi hilo kama shambulio katika ardhi yake. Israel ilidai kuwa majengo hayo hayajalindwa na mikataba ya kidiplomasia kwani Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran limeyageuza kuwa kituo cha kijeshi.
Hiyo ilikuwa hatua nyingine yenye hatari kubwa.
Ikiwa shambulio la Isfahan halitafuatiwa na mashambulizi zaidi, basi mvutano huo utapungua .
Kilichotokea mara moja kinaweza kuwa jaribio la Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kujibu, bila kumtenga Bw Biden zaidi ya vile alivyokuwa tayari.
Ikiwa ndivyo hivyo, swali lingine ni iwapo itatosha kwa majenerali wa zamani katika baraza la mawaziri la vita la Israel ambao wanaaminika kutaka jibu kali, kama wanavyoona, kurejesha uwezo wa Israel kuwazuia maadui zake.
0 Comments