Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Bodi ya wakurugenzi Chuo cha uongozi cha ESAMI kilichopo Njiro jijini Arusha, chini ya Mwenyekiti Simon Masanga (Zimbabwe),imemwondoa madarakani Mkurugenzi wa uchumi na fedha Prof Martin Lwanga bila kufuata sheria za ajira na haki za binadamu.
Masanga , anatuhumiwa kuzuia ukaguzi unaohusisha upotevu wa dola 50,000 za kimarekani katika chuo hicho jambo ambalo bodi hiyo kwa kushirikiana na menejimenti ya utawala ilimwondoa Mkurugenzi huyo raia wa Zimbabwe.
Prof Lwanga ameshika madaraka hayo chuoni hapo kwa muda wa mwaka mmoja na kufanya mabadiliko makubwa ikiwemo kuinua mapato ya chuo hicho kwa asilimia 13% ya mapato ya mwaka 2022, kubana matumizi yasiyo ya lazima,kujumuisha Watanzania kwenye menejiment ya Chuo jambo ambalo hapo awali halikuwepo.
Pia alipigania maslahi ya wafanyakazi ikiwemo nyongeza ya mshahara, kuinua kima cha chini cha mshahara kwa asilimia 200%, kuongeza posho ya Elimu kwa watoto wa wafanyakazi kwa asilimia 100%, kubadilisha miundombinu ya mwaka 1980 na kuweka ya kisasa pamoja na kujenga geti la kisasa linaloitambulisha ESAMI.
Kuendeleza ujenzi wa jengo la ESAMI nchini Malawi, kuzuia matumizi mabaya ya kinga ya kidiplomasia (prevention of abuse of iplomatic immunity )
Sipho Limbe Mwanasheria
Dr Chengatai Magunje
Prof Joseph Mumba Mwakilishi wa wafanyakazi ESAMI
Dr David Kalaba Mkurugenzi wa fedha na utawala
Prof Simon Masanga Mw/kiti wa Bodi
Dr Chengatai Magunje
Prof Joseph Mumba Mwakilishi wa wafanyakazi ESAMI
Dr David Kalaba Mkurugenzi wa fedha na utawala
Prof Simon Masanga Mw/kiti wa Bodi
Kwa kifupi kuna sababu nne au tano zilizosababisha kuondolewa Prof Martin Lwanga bila kufuata utaratibu.
1. Uamzi wa Prof Martin Lwanga kujumuisha Watanzania kwenye menejimenti ya ESAMI.
2. Uamuzi wa Prof Martin Lwanga kufanya mabadiliko MAKUBWA kwenye masilahi ya wafanyakazi, kuwekeza kwenye miundo mbinu na kuinua kiwango cha chini cha mishahara.
3. kufanikisha lengo la watuhumiwa wa wizi wa dola 50,000 kuzuia ukaguzi (Forensic audit) na utakatishaji wa dola za Kimarekani 50,000
iv. Utawala uliopita wa Prof Bonard Mwape kulinda masilahi yao.
v. Kulinda matumizi mabaya ya ofisi ya Mwenyekiti wa bodi na Mwanasheria wa ESAMI.
Maelezo kamili yanafuata hapa chini;
1) Uamzi wa Prof Martin Lwanga kujumuisha Watanzania kwenye menejimenti ya ESAMI
Prof Martin Lwanga alikuta menejimenti yote ya Utawala wa Prof Bonard Mwape ilikuwa ya wageni tu bila hata Mtanzania mmoja, kitu ambacho aliona sio sahihi na akaamua kubadilisha na kuongeza Watanzania wawili Bw Leon Malisa na Prof Dr Luck Yona.
Uamzi huu wa kuendelea na menejimeti ya mtangulizi wake pamoja na kuongeza hao Watanzania wawili ilimuletea upinzani mkubwa sana kwa sababu iliharibu mipango yao ya ufisadi.
2). Uamzi wa Prof Martin Lwanga kufanya mabadiliko kwenye masilahi ya wafanyakazi, kuwekeza kwenye miundo mbinu na kuinua kima cha chini cha mishahara.
Alipooanza kazi, Prof Martin Lwanga alianza kwa kufanya mikutano na makundi yote ya wafanyakazi ili kujua mawazo ya wafanyakazi wote bila kubagua.
Kutokana na mikutano hiyo alipata taarifa za mambo mengi mabaya ambayo hayakufanywa vizuri na utawala uliopita ikiwemo pengo kubwa la mishahara (massive salary inequality), wafanyakazi kutoenda likizo, pengo kubwa la ada za watoto wa wafanyakazi wanaolipiwa na Chuo.
Ukosefu wa vitendea kazi, miundombinu ya chuo iliyochakaa, unyanyasaji wa wafanyakazi, unyanyasaji wakijinsia na wajawazito na matumizi mabaya ya kinga ya kidiplomasia (abuse of diplomatic immunity).
Baada ya kukusanya maoni ya wafanyakazi alianza kufanya mabadiliko jambo ambalo halikuwafurahisha baadhi ya wajumbe wa utawala uliopita hadi kukimbilia kwa Mwenyekiti wa Bodi Bw Simon Masanga (Zimbabwe) kumshitaki kwa kile walichokiita ‘matumizi mabaya’ ya pesa.
Mojawapo ya mabadiliko aliyoyafanya ndani ya mwaka mmoja wa utawala wake ni kama ifuatavyo; kuongeza mapato ya chuo kwa asilimia kumi na tatu (13%) ya mapato ya mwaka 2022, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuongeza mishahara ya wafanyakazi na kupandisha kima cha chini cha mshahara kwa asilimia mia mbili (200%).
Alitoa amri wafanyakazi wote kwenda likizo tofauti na utawala uliopita uliokuwa unazuia watu kwenda likizo, kuhusu unyanyasaji wa kijinsia, Prof Martin Lwanga alikemea unyanysaji na kuunda kamati ya staff Welfare ili kupokea malalamiko ya wafanyakazi.
Upande wa miundombinu, Prof Martini Lwanga alianza kwa kuweka taa za barabarani, CCTV camera, kuweka barabara marumaru (paving), kuchimba visima ili kuanza umwagiliaji (garden).
Kutengeneza geti la mfano linalotangaza chuo, kuondoa mifumo ya vyoo vya mwaka 1980 na kuweka mifumo ya kisasa, kuboresha vitendea kazi, lengo likiwa (kama alivosema mwenyewe) makao Makuu ya ESAMI yaendane na hadhi ya Chuo.
Kuhusu matumizi mabaya ya kinga ya kidiplomasia, Prof Martin Lwanga alipokea taarifa kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya kinga ya diplomasia kipindi cha utawala uliomaliza muda, alitoa onyo juu ya matumizi mabaya ya kinga ya kidiplomasia (Diplomatic immunity) na kuahidi kuwa hatavumilia vitendo hivyo.
Kila alipojaribu kutekeleza hayo yote alijikuta ametengeneza maadui waliokuwa wamezoea kula pesa za chuo kwa manufaa yao bila kujali mstakabari wa chuo. Miongoni mwa watu waliopambana kumkwamisha Prof Martin Lwanga ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.
Dr David Kalaba ( Zambia), Mkurugenzi wa Masoko na Biashara Dr, Chengetai Magunje (Zimbabwe), na Mwakilishi wa wafanyakazi kwenye Bodi , Prof Joseph Mumba (Malawi), Mkurugenzi wa MBA.
Dr, Peter Kiuluku (Kenya) na wakili Sipho Limbe ( Malawi). Watu hao waliungana na Mweneyekiti wa Bodi Bw Simon Masanga (Zimbabwe), na kuanza mbinu za kumtoa Prof Martin Lwanga Madarakani bila kufuata utaratibu (serious abuse of office power).
3). Lengo la Utawala uliopita kuzuia ukaguzi wa wizi (Forensic audit) na utakatishaji wa dola za Kimarekani 50,000
Menejimenti ilimweleza Prof Martin Lwanga kuwa kuna malalamiko ya ubadhilifu wa dola za kimarekani 50,000 keshi iliyochukuliwa na Mkurugenzi wa Fedha Dr David Kalaba mwezi October 2022.
Kwa kutumia barua pepe bila nyaraka zinazoonyesha pesa hizo nizanini na bila kuonyesha mpokeaji wa pesa hizo ni nani. Taarifa hiyo ilimfanya Prof Martin Lwanga kwenda Bodi kuomba ruhusa ya kufanya ukaguzi wa hali ya kifedha ya chuo pamoja na kuchunguza (forensic audit) ubadhilifu wa dola za kimarekani 50,000 mali ya chuo.
Dr. David Kalaba (Zambia), Mkurugenzi wa Fedha na Utawala waESAMI alichukua dola 50,000 za Marekani mali ya Chuo kwa kutumia email, alikula njama moja na Mwenyekiti wa Bodi Simon Masanga ili ampandishe cheo kuwa Deputy Director General ili kuzuia uchunguzi wa wizi dhidi yake.
Pia, alimshawishi mwenyekiti wa Bodi Bw Simon Masanga kuzuia ukaguzi (Forensic Audit) wa wizi wa dola 50,000 mali ya chuo.
Alishirikiana na Mwanasheria wa Chuo Bw Sipho Limbe (Malawi) kuandaa mashitaka ya uongo dhidi ya Prof Martin Lwanga ili aondolewe na kuwa huru dhidi ya uchunguzi wa wizi. Ni mhusika mhimu katika kutakatisha dola za kimarekani 50,000 mali ya chuo.
Kwa mshangao wa menejimenti na wafanyakazi wa Chuo cha ESAMI, Bodi chini ya Mwenyekiti wake Simon Masanga (Zimbabwe) ilizuia uchunguzi (Forensic audit) ya dola za kimarekani 50,000 isifanyike pamoja na uchunguzi wa hali ya kifedha.
Kutokana na mazingira ya kutokabidhiwa ofisi na mtangulizi wake, na hivyo kutojua hali ya kifedha na madeni ya Chuo, Prof Martin Lwanga aliona ni mhimu kujua hali ya chuo kifedha.
Hivyo menejiment iliamua kuunda kamati iliyoundwa na wastaafu wa ESAMI (retirees, Dr Jonathan Kilimba , ACPA John Majo, CPA Dr Peter Mitiambo pamoja na mfanyakazi mwandamizi CPA Felix Kamau) ili kumsaidia kujua hali ya kifedha ya Chuo na ukweli wa ubadhilifu huo.
Report ya kamati ilionyesha kuwa ni kweli kuna Dola za kimarekani 50,000 zilizochukuliwa na Dr David Kalaba bila kufuata utaratibu na kukosekana kwa nyaraka muhimu za mnufaika wa pesa hizo.
Kutokana na uchunguzi huo Dr David Kalaba alikubali kupokea pesa hizo na kumpa Mkuu wa masoko na Biashara, Dr Chengetai Magunje.
Dr. Chengetai Magunje (Zimbabwe) alishirikiana na Mwenyekiti wa Bodi Simoni Masanga (Zimbabwe) ili kupeleka mashitaka ya uongo dhidiya Prof Martin Lwanga, Pia anatuhumiwa na Mkurugenzi wa Fedha Dr David Kalaba kupokea dola 50,000 za Marekani, ambazo hadi sasa hazijulikani ziliko, anatuhumiwa kutakatisha dola $50,000 mali ya chuo.
Taarifa ya kamati iliungwa mkono na wakaguzi wa mwisho wa mwaka (annual audit) ambao walisema kwa kweli hela ilitoka bila kufuata utaratibu na kukosa nyaraka muhimu.
Baada ya matokeo ya report hiyo, Mkurugenzi wa Fedha Dr David Kalaba (Zambia) anayetuhumiwa kwa ubadhilifu alikimbilia kumshitaki Prof Martin Lwanga (DG) kwa Mwenyekiti wa Bodi Bw Simon Masanga (Zimbabwe) kwa kukiuka maelekezo ya Bodi ambao ndio waajiri wake.
Kwa mshangao wa wafanyakazi na menejiment, Mwenyekiti wa Bodi Bw Simon Masanga (Zimbabwe), alichagua kulinda ubadhilifu wa fedha za Chuo cha ESAMI na kuungana na mshukiwa wa ubadhilifu Dr David Kalaba.
Toka wakati huo, Mwenyekiti wa Bodi, Bw Simon Masanga aliendelea kushirikiana na Mkurugenzi wa fedha Dr David Kalaba ili kumkwamisha Prof Martin Lwanga (DG) katika kila alichokifanya hadi kumsimamisha kazi na mwisho kumfuta kazi bila kupewa haki yake ya kusikilizwa.
4). Utawala uliomaliza muda wake wa Prof Bonard Mwape kulinda masilahi yao.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mwenyekiti wa Bodi,Simon Masanga (Zimbabwe), ambaye ni msimamizi wa utawala bora na kuzuia rushwa mahali pa kazi alichagua kuwapandisha vyeo wafanyakazi waliompelekea malalamiko kwa simu na hivyo kuwazawadia vyeo Dr Peter Kiuluku kuwa Acting Director General na Mtuhumiwa namba moja wa ubadhilifu wa dola za kimarekani 50,000 Dr David Kalaba kuwa Deputy Director General ( nafasi hii haikuwepo kwa miaka yote 24 ya Prof Bonard Mwape).
Kitu ambacho ni kinyume na kanuni za utawala bora, uadilifu, kinga ya kidiplomasia, na maadalili ya kazi.
Dr. Peter Kiuluku ni mhusika mkuu katika mipango ya kumuondoa madarakani Prof Martin Lwanga bila kufuata sheria za kazi (labour law) amekuwa kwenye menejimenti ya Prof Bonard Mwape kwa miaka 15, kama ahsante, alizawadiwa cheo na Mwenyekiti wa Bodi Bw Simon Masanga kuwa Acting Director General, alitumiwa na Mwenyekiti wa Bodi Bwana Simon Masanga kufukuza wafanyakazi wawili bila kuwasikiliza wala kufuata sheria za kazi.
Ametoa vitisho (intimidation) vya kufukuza mfanyakazi yeyote atakayepinga maamuzi ya Mweneykiti wa Bodi Bw Simon Masanga kumpandisha cheo na kuwa Acting Director General.
5). Kulinda matumizi mabaya ya ofisi ya Mwenyekiti wa bodi na Mwanasheria wa ESAMI.
a) Ofisi ya mwenyekiti wa bodi kuingilia utendaji kazi wa menejimenti ya ESAMI..
Kazi kubwa ya Bodi zote duniani ni kusimamia mipango mkakati ya kampuni (strategic and corporate governance issues), lakini katika hali isiyo ya kawaida.
Mwenyekiti wa Bodi Bwana Simon Masanga (Zimbabwe) kupitia kwa Acting Director General Dr Peter Kiuluku na Mwakilishi wa wafanyakazi kwenye Bodi Prof Joseph Mumba mapema mwezi wa nne (Aprili 2024) aliwafuta kazi wafanyakazi wawili ambao hawaripoti kwenye Bodi, na kutoa barua za kuwaachisha kazi.
Kama sehemu ya vitisho (intimidation) aliahidi kuwafukuza kazi wafanyakazi wote watakaopinga maamuzi yake yasiyofuata utaratibu ya kumfuta kazi Prof Martin Lwanga na kuwapandisha vyeo watuhumiwa wa uchochezi na ubadhilifu Dr Peter Kiuluku na Dr David Kalaba kitu ambacho sio kazi ya Bodi lakini ni kazi ya menejimenti.
Katika tukio lingine, tarehe 04.03.2024 mwakilishi wa wafanyakazi kwenye Bodi, Prof Joseph Mumba, aliwaeleza wafanyakazi kuwa yeye hakuwahi kupeleka mashitaka yoyote Bodi dhidi ya Prof Martin Lwanga.
Akiwa kwenye kikao cha Bodi mwezi Disember 2023, Namibia alishuhudia Mwenyekiti wa bodi, Bw Simon Masanga (Zimbabwe) akisoma mashitaka dhidi ya Prof Martin Lwanga kutoka kwenye simu yake na kuyafanya kuwa agenda ya kikao, kitu kinachoonyesha ameweka watu wake ndani ya chuo kwa kumpa taarifa zisizo sahihi kuhusu Prof Martin Lwanga.
Prof. Joseph Mumba (Malawi),Mwakilishi wa Wafanyakazi kwenye Bodi, alikuwa mshindi wa pili kwenye usaili ilyiomuweka madarakani Prof Martin Lwanga, anakana kuhusika kupeleka mashitaka Bodi dhidi ya Prof Martin Lwanga, na kwamba mashitaka dhidi ya Prof Martin Lwanga yalikuwa ya Mwenyekiti wa Bodi Bw Simon Masanga aliyasoma kwenye simu, alishirikiana na Mwanasheria wa Chuo Bw Sipho Limbe (Malawi) na kutoa lugha za vitisho kwa walinzi wa geti na watu wa mapokezi na kuwataka wamzuie Prof Martin Lwanga kurudi ofisini.
A) Alitangazia wafanyakazi kufuta kazi kila mtu atakayepinga maamuzi ya kumfuta kazi bila utaratibu Prof Martin Lwanga. Aliunga mkono kufukuzwa kwa wafanyakazi wawili bili kuwasikiliza.
Utaratibu sahihi wa Chuo Cha Kidiplomasia Cha ESAMI, hupokea malalamiko ya wafanyakazi kupitia kwenye kamati ya Staff Welfare au mkutano wa wafanyakazi na kupelekwa kwa Mwakilishi wa wafanyakazi kwenye Bodi.
Katika kipindi hicho Hakuna mkutano wa wafanyakazi uliofanyika wala kamati ya Staff welfare haikupokea malalamiko yoyote kutoka kwa wafanyakazi kuhusu Prof Martin Lwanga.
Kitendo hicho cha Mwenyekiti wa Bodi kujifanya yeye ndio anajua matatizo ya wafanyakazi (operational) kuliko wafanyakazi wenyewe si tu kinaonyesha mazingira ya rushwa pia kinamvunjia heshima kama Mwenekiti wa Bodi wa chuo chenye hadhi ya ESAMI.
B). Ofisi ya mwenyekiti wa bodi kutumika kudhalilisha mkurugenzi wa chuo cha ESAMI, Prof Martin Lwanga.
Pamoja na kuwa ofisi ya Mwenyekiti wa Bodi ilipanga tarehe ya kikao mwezi mmoja kabla, tarehe hiyo ilifichwa na kuwa siri. Hali iliyopelekea mwaliko kumfikia Prof Martin Lwanga masaa 12 kabla ya kikao bila kujali umbali wa safari kutoka Arusha kwenda Nairobi (Km 284).
Utharirishaji wa namna hii wa Mwenyekiti wa Bodi Bw Simon Masanga kwa Mkurugenzi wa ESAMI Prof Martin Lwanga haukubariki.
C). Ofisi ya mwenyekiti wa bodi na ofisi ya mwakilishi wa wafanyakazi kwenye bodi iliungana na mwanasheria wa chuo kuandaa mashitaka ya uongo dhidi ya Mkurugenzi wa ESAMI Prof Martin Lwanga.
Katika hali ya mshangao kwa wafanyakazi, mwanasheria anayeripoti kwa Mkurugenzi Prof Martin Lwanga aligeuka na kuwa mwanasheria wa ofisi ya mwenyekiti wa Bodi.
Hali hii ilisababisha Mwanasheria na Mwenyekiti wa Bodi Bw Simon Masanga kupanga mipango kumuondoa madarakani Prof Martin Lwanga bila kufuata sheria.
Mnamo tarehe 04.03.2024.
Mwanasheria wa chuo Sipho Limbe (Malawi), akiambatana na Mwakilishi wa wafanyakazi kwenye Bodi Prof Joseph Mumba (Malawi), walikwenda geti la chuo na kutoa vitisho kwa walinzi na kuwaonya wasijaribu kumfungulia geti Prof Martin Lwanga kuingia ofisin. Kitendo hicho cha uvamizi ni kinyume na makataba wake wa kazi.
Sipho Limbe (Malawi), Mwanasheria aliyeshauri Bodi kuzuia ukaguzi wa wizi wa dola za kimarekani 50,000 kinyume na miiko ya taaluma ya sheria, alihusika kutoa lugha za vitisho (intimidation) dhidi ya wafanyakazi wa Mapokezi na Walinzi na kuwataka kumzuia Prof Martin Lwanga kurejea ofisini.Aligeuka na kuwa mwanasheria wa Mwenyekiti wa Bodi Bw Simon Masanga kinyume na mkataba wa kazi. Ni mhusika mkuu wa kuandaa mashitaka ya uongo dhidi ya mwajiri wake Prof Martin Lwanga kinyume na mkataba wake wa kazi.
HISTORIA YA CHUO CHA ESAMI
ESAMI ni Chuo cha Kidiplomasia kilichoanzishwa mwaka 1980, na kinachomilikiwa na nchi kumi (10), Arusha (Tanzania) ikiwa makao makuu. Chuo hiki kilikuwa mali ya nchi za Afrika mashariki (EAC, Tanzania, Uganda and Kenya).
Baadaye kwenye mkutano wa OAU, uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia walizikaribisha nchi saba za kusini mwa bara la Afrika (Msumbiji, Malawi, Zambia, Seychelles, Eswatini, Namibia na Zimbabwe) na kupata jina la Eastern and Southern African Management Institutte (ESAMI).
Bodi ya ESAMI inaundwa na Makatibu Wakuu wa Utumishi wa kila nchi mwanachama, ambao huchagua Mwenyekiti wa Bodi ambaye kwa sasa ni Bw Simon Masanga (Zimbabwe) picha yake hapo.
Simon Masanga (Zimbabwe) Mwenyekiti waBodi yaESAMI anayetuhumiwa kuzuia ukaguzi wa wizi wa dola $50,000 na kuungana na menejimenti ya utawala uliyopita kumpindua Mkurugenzi Mkuu wa ESAMI bila kufuata sheria za kazi na kuwazawadia vyeo wafanyakazi waliomtumia meseji za malalamiko.
WAKURUGENZI WA CHUO CHA ESAMI (DIRECTOR GENERAL).
Hadi kufikia sasa chuo cha Kidiplomasia cha ESAMI kimetawaliwa na wakurugenzi watano, kutoka Kenya (2), Zambia (2) na Uganda(1). Mkurugenzi hupatikana miongoni mwa nchi wanachama kwa kupitia utaratibu shindani wa ajira.
Prof Bonard Mwape (Zambia) ndiye Mkurugenzi aliyetawala kwa muda mrefu wa miaka 24 mfululizo kinyume na mkataba ulioanzisha Chuo cha ESAMI inayotaka kila Mkurugenzi kutumikia vipindi viwili vya miaka mitano tu.
MIZENGWE KATIKA KUMPATA PROF MARTIN LWANGA.
Tofauti na utaratibu uliozoeleka, mizengwe ilianza na tangazo la mwezi July 2022 la nafasi ya mkurugenzi kwa kutaja sifa ya mtu kuwa asiye na miaka 60 na mwenye kiwango cha Elimu ya MBA, kinyume na matakwa ya mkataba wa kuanzishwa chuo.
Tangazo hilo lililaumiwa na wafanyakazi wote kwa vile lililenga kumuondoa Mtanzania Prof Dr Lucky Yona aliyekuwa anafikisha miaka 60 na kuonyesha tangazo hilo lilimlenga Mwana Mama Dr Chengetai Magunje aliyekuwa na Elimu ya MBA pamoja na umri wake kuwa chini ya miaka 60.
Dr Chengetai Magunje alikuwa mtu wa karibu na mkurugenzi Prof Bonard Mwape. Baada ya malalamiko hayo tangazo hilo lilibadilishwa na kufuta kigezo cha miaka 60 na Elimu ya MBA likaweka sharti mtu awe ni professor au Dakitari mwenye uzoefu wa miaka kumi katika utumishi wa juu.
KUITWA KWENYE USAILI.
Bodi ilipitisha majina matano ya wagombea wa kiti cha Mkurugenzi (Director General) kutoka Tanzania (1), Kenya (2), Uganda (1) na Malawi (1) huyu ndio mfanyakazi wa ndani aliyefanikiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro. Baada ya usaili, watu wawili walipenya na kuingia kwenye namba mbili za juu ambao ni,
1. Prof Martin Lwanga (Uganda)
2. Prof Joseph Mumba (Malawi) mhadhiri pekee wa ESAMI aliyeingia katika kinyang’anyiro cha watu watano, na aliyepigiwa chapuo na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake.
Bodi ya ESAMI ilimtangaza Prof Martin Lwanga (Uganda) kuwa mshindi wa nafasi ya Mkurugenzi wa tano wa Chuo cha Kidiplomasia cha ESAMI, Disemba 2022.
Prof Martin Lwanga aliripoti kazini mwezi Februari 2023 na kukabidhiwa ofisi na Kaimu (‘caretaker’). Mtangulizi wake Prof Bonard Mwape hakufika kumkabidhi ofisi.
0 Comments