Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
Dereva wa basi lililouwa WANAFUNZI 8 na raia mmoja wa shule yenye mchepuo wa kiingereza ya Ghati Memorial, Lukuman Hemedi, amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka nane likiwemo la kuua bila kukusudia.
Dereva huyo ambaye baadaye aliomba apelekwe gerezani kukwepa hasira za wananchi, alisomewa mashtaka hayo na wakili wa serikali Amina Kiamba, mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya, Sheila Mamento.
Kesi hiyo imeahirishwa Hadi Aprii 30,2024 itakapokuja tena mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa baada ya wakili wa serikali kuiambia mahakama hiyo upelelezi bado haujakamilika.
Hata hivyo hakimu alisema kuwa dhamana kwa mshtakiwa IPO wazi lakini wakili wa serikali aliiomba mahakama imnyime dhamana kwa madai akiachiwa anaweza kudhulika na hasira za wananchi, ndipo hakimu alipomhoji mshtakiwa kama anakubaliana na ombi hilo ambaye naye alikubali na kusema nakwenda gerezani.
Tukio hilo lilitokea April 12 mwaka huu majira ya saa 12.30 asubuhi baada ya gari hilo aina y aToyota Haice lenye namba T 496 EFL Mali ya shule hiyo likiwa na wanafunzi 13 kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo lenye maji kasi na kusababisha vifo vya wanafunzi 8 na Msamalia Mmoja.
Ends
0 Comments