BREAKING! AICC YATIKISWA,VIGOGO WAZITO WASIMAMISHWA KAZI KWA UBADHILIFU,WANATUHUMIWA KUTAFUNA MAMILIONI KAMA MCHWA,YUMO MKURUGENZI MKUU WA FEDHA,AKIRI KUPOKEA BARUA

Aicc yatikiswa , vigogo wazito wasimamishwa kazi  kwa kutafuna mamilioni ya fedha kama Mchwa,Yumo Mkurugenzi Mkuu wa fedha  ,SAVO MUNG'ONG'O.

Na Joseph Ngilisho ARUSHA

VIGOGO sita wa Ngazi za juu wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa  cha Arusha (AICC)na kituo cha  JNICC Dar es salaam, wamesimamishwa kazi kwa kile kinachodaiwa ni Ubadhilifu Mkubwa wa mamilioni ya Fedha na kufanya kituo hicho kushindwa kujiendesha kwa faida ikiwemo kutoa gawio serikalini kwa muda mrefu.

Taarifa za uhakika toka ndani ya Aicc ambazo mamlaka husika imezifanya siri, zinadai kuwa ,Bodi ya Aicc ndio imewasimamisha kazi vigogo hao kwa maslahi mapana ya umma baada kubaini wamekuwa chanzo cha upotevu wa mapato kwa ubadhilifu wa kutisha, na kwamba kiasi cha upotevu bado kinachunguzwa.

Waliosimamishwa kwa tuhuma za kuhujumu mapato ya kituo hicho ni pamoja na Savo Mung'ong'o ( mkurugenzi wa fedha na utawala Pia alikaimu nafasi ya ukurugenzi baada ya aliyekuwa mkurugenzi Eliashilia kaaya kufariki dunia )

2. Mkunde Mushi  , huyu ni mkurugenzi wa mikutano na masomo


2. Victor Kamagenge ,huyu ni mkurugenzi wa miliki na miradi


4. Aigostine Stanislaus karadoga , mhasibu mkuu wa shirika


5. Festo fanuel Mramba  ,huyu ni mkuu wa rasilimali watu


6. Catherine kilinda , huyu ni meneja wa kituo Cha mikutano dar es salaam ( JNICC)

Afisa habari wa Aicc na mkuu wa itifaki, Fredrick Maro alipoulizwa juu ya taarifa hizo alishindwa kukataa ama kukubali na badala yake alisema hajajiandaa kutoa taarifa hiyo japo awali alionesha nia na kutaka apatiwe Email ya Mwandishi ili amtumie taarifa yenye ufafanuzi wa kina wa jambo hilo.

Mkurugenzi Mpya wa Aicc,Christine Mwakatobe ambaye March 18,mwaka huu aliteuliwa na Rais Samia na Marchi 22 alitambulishwa kituoni hapo,alisema jambo hilo hata yeye analisikia ila hajalijua kiundani kwa kuwa yeye ni Mpya katika kiti hicho na kutaka atafutwe msemaji wa kituo.

Christine Mwakatobe Mkurugenzi Mwendeshaji AICC

"Ni kweli hata mimi nimelisikia ila sijajua undani wake si unajua mimi ni mgeni katika wadhifa huu slila watafute wasemaji wa Aicc watakuambia"

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Aicc,Begum Tajada alipoulizwa alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa sasa na kuomba apewe muda wa wiki mbili ndipo atalitolea ufafanuzi

"Siwezi kuzungumzia suala hilo kwa sasa naomba unipe muda kama wiki mbili hivi"

Mmoja ya vigogo waliosimamishwa kazi,Savo Mung'ong'o Mkuruhenzi wa Fedha ,alipohojiwa alikiri kupokea barua ya kusimamishwa kazi na kudai  kwamba hadi sasa hajui chochote juu ya tuhuma zake na amekaa pembeni akisubiri kuambiwa Madhambi yake.

"Nikweli nimepokea barua ya kusimamishwa kazi na hadi sasa sijui tuhuma zangu, mimi na wenzangu tunasubiri kuambiwa  tuhuma zetu"alisema Mung'ong'o wakati akihojiwa kwa njia ya simu.

Ends..






















Post a Comment

0 Comments