13 WAFA KWA AJALI MBAYA YA HIACE NA LORI LA MAFUTA

 By Ngilisho Tv 

Watu 13 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace lililokuwa likitokea Somanga kuelekea Kilwa Mkoani Lindi kugongana uso kwa uso na lori la mafuta leo April 22,2024 katika Kijiji cha Somanga.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika barabara kuu ya Lindi - Kibiti ambapo amesema chanzo cha ajali ni Dereva wa lori kuhama upande wake na kuingia upande wa Hiace na kugongana uso kwa uso.


Majeruhi sita wanapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Tingi huku miili ya waliofariki ikihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya  Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.


Kamanda Imori amesema Mashuhuda wamesema Dereva wa lori amelewa na walimuona akiwa anayumba na kumgonga Mwendesha baiskeli kabla ya ajali hyo ya gari, hivyo atafanyiwa vipimo na ikibainika alikunywa pombe kupita kiasi atachukuliwa hatua “Dereva wa lori na wa Hiace wote tumewakamata kwa mahojiano”

Post a Comment

0 Comments