TAZAMA WANYAMA WANAVYOANGAMIA KWA KUGONGWA MIKUMI, ZAIDI YA 300 HUFA KILA MWAKA ,KAMERA ZA KISASA KUFUNGWA KUDHIBITI MATUKIO,'UKIUA TEMBO NA TWIGA FAINI DOLA 20,000'

Na Joseph Ngilisho-MOROGORO 

Wanyama zaidi ya 300 wa aina tofauti katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi,Mkoani Morogoro, hufa kila mwaka  kwa kugongwa na magari katika barabara kuu ya Morogoro-Iringa hadi Zambia inayopita katikati ya hifadhi hiyo kwa kipande cha kilometa 50 na kusabahisha hasara ya  bilioni 6. 


Akiongea na waandishi wa habari waliombelea hifadhi hiyo Mkuu wa hifadhi hiyo, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, ACC,Agustino Masesa ,alisema vifo vya wanyama hao vinatokana na ukaidi wa madereva wasiotaka kuzingatia sheria za uhifadhi licha ya elimu wanayopewa.

Alisema kipande cha barabara kinachopita kwenye hifadhi hiyo chenye urefu wa kilomita 50,kimewekwa alama zote za utambuzi yakiwemo mabango, lakini baadhi ya madereva wanapita kwa mwendo wa kasi unaoathiri  wanyama,miundo mbinu na uharibifu wa Magari .


"Ili kukabiliana na hali hiyo tumeamua kufunga Kamera za kisasa zitakazosaidia kufuatilia mwenendo wa magari na kuchukua hatua kali na faini yetu itakuwa kubwa kidogo".


Masesa alibainisha wanyama wanaogongwa mara kwa mara kuwa ni Swala Pala ambao huruka kwa wastani wa 15 hadi 20, Simba,Chui, Twiga,

Tembo, Nyani, Nguruwe, Digidigi na matukio hayo zaidi hutokea nyakati za usiku. 

Wakati huo huo Masesa alisema , hifadhi hiyo imekuwa na ongezeko la watalii wanaotokea visiwa vya Zanzibar ambapo kila siku watalii wapatao 200 hadi 250 wanatembelea  hifadhi na ndege 10 hadi 15 zinatua kila siku kuleta watalii katika hifadhi hiyo. 


Alisema ongezeko hilo limewezesha hifadhi hiyo kukusanya mapato yanayofikia kiasi cha sh, bilioni 6 kwa mwaka na mkakati ni kufikisha mapato ya sh,bilioni 10 ifikapo 2025.






"Kwa sasa tupo katika hatua ya kupanua uwanja wetu wa ndege kwa kuboresha miundo mbinu ili kuruhusu ndege kubwa kutua  na ndani ya miezi miwili uwanja huo utakuwa tayari na tutakuwa na uhakika wa kupokea ndege zaidi ya 50 zikiwemo ndege kubwa"


Masesa aliwakaribisha wawekezaji kwenda kuwekeza ujenzi wa vyumba vya kulaza wageni kwa kuwa anauhakika baada ya maboresho wanayoyafanya kwa sasa pamoja na matangazo mbalimbali watapokea wataii si chini ya 400 kila siku.


Naye mhasibu Mkuu hifadhi ya mikumi Buka Mwankisye alisema katika kipindi cha miaka mwili julai 2022 hadi Julai 2023 walitoza faini za makosa ya kugonga wanyama ,mwendo kasi na uchafuzi wa mazingira zinazofikia kiasi cha shilingi 113.2.

Buka, Mhasibu Mikumi

"Kutokana na kutozwa kwa faini matukio ya kugonga wanyama yamepungua ,katika kipindi cha mwaka 2023/24 faini iliyotizwa ni kiasi cha sh,milioni 42.3 tu hii ni kutokana na elimu tunayotoa na faini zetu  kwa mnyama Tembo na Twiga ni dola 20,000  ,Simba dola 7000,Nyani dola 150,Swala dola 390,Punda milia dola 1200 , Nyumbu dola 650 na digidigi dola 300"


Pia alisema mapato  ya Hifadhi hiyo yamepanda kutoka mwaka wa fedha 2020 na 2021 hifadhi ilikusanya sh,bilioni 1 6 baada ya kupokea wageni 45,677 ,mwaka 2021/22 mapato yalikuwa bilioni 2.5 baada ya kupokea wageni 66,790 sawa na ongezeko la asilimia 51 .


Alisema mwaka wa fedha 2022/23 walipokea wageni 109,000 na kukusanya mapato ya sh,bilioni 4.6 sawa nanongezeko la asilimia 86 na mwaka huu wa fedha 2022/24 wageni ambao wameingia hadi sasa ni 101,000 na kiasi cha sh, bilioni 4.8 sawa na ongezeko la asilimia 6 kimeshakusanywa .



Awali afisa uhifadhi ,Fatuma Mcharazo alisema hifadhi ya Mikumi ilianzishwa mwaka 1964 ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 3230 na kupakana na wilaya za Mvomelo,Kilosa na Morogoro ikiwa na vivutio vya ndege wa aina zaidi ya 400 na wanyama wote wakubwa kasoro nyati ambao walitoweka miaka ya nyuma kwa sababu ya matukio ya ujangili.


Alisema,hifadhi hiyo inavivutio vingi ikiwemo misitu minene ,maporomoko ya maji ya Udzungwa,mabwawa ya viboko na alitumia wasaa huo kuwataka watalii wa ndani kutoka mikoa ya Iringa ,Dar es salaam na Mbeya kuzitumia sikukuu za Pasaka na Idd  kutembelea hifadhi hiyo na kujionea vivutio hivyo.


Ends..









Post a Comment

0 Comments