WAFANYABIASHARA ARUSHA WACHEKELEA RC MONGELA KUNG'OLEWA,WASEMA MAKONDA NI TUMAINI LAO ATAENDANA NAO,WADAI ALIWATESA SANA,ALIPANGA KUBOMOA VIBANDA VYAO KISA GAMBO ANAWASAPOTI

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Wafanyabiashara wajenzi wa Maduka stend Ndogo jijini Arusha wamempongeza rais Samia Suluhu Hasani kwa kufanya mabadiliko ya uongozi kw kumwondoa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela wakidai alichangia mgogoro kati yao  na Halmashauri ya jiji la Arusha.

Aidha wamemwomba Rais Samia kuvunja baraza La madiwani la jiji hilo, wakidai limekuwa likitumika vibaya katika maamuzi yake  ikiwemo tetezi za kuruhusu kuvunjwa kwa maduka yao ili kuruhusu uwekezaji usio na tija.

Pia wamempongeza Mkurugenzi wa jiji la Arusha ,Mhandisi Jumaa Hamsin, kwa kusimamia vema mapato ya serikali wakidai kuwa awali mkurugenzi huyo alikuwa akiyumbishwa na mkuu huyo wa Mkoa ila sasa wanaamini atasimama kwa miguu yake mwenyewe kutenda haki katika maamuzi yake kwa maslahi mapana .

Akiongea kwa njia ya simu Mwenyekiti wa wilaya wa wafanyabiashara Arusha,Dominic Mollel alisema kitendo cha  Mongela  kuondolewa Arusha na kuletwa kwa RC Mpya Paul Makonda kimerejesha  mioyo iliyovunjika vipande vipande  ya wafanyabiashara .

Alisema kuwa katika kipindi chote Mongela akiwa mkuu wa Mkoa wameishi kwa misukosuko mikubwa na hivi sasa inadaiwa eneo hilo aliagiza lipewe  mwekezaji na vibanda vyao vibomolewe.

"Mimi namshukuru sana rais kwa kuona kilio cha wafanyabiashara na kuamua kumwondoa MONGELA ARUSHA, kwa sababu wafanyabiashara wameteseka sana bila kujali kazi aliyotumwa na wananchi,ameweza kuruhusu uwekezaji eneo la stendi ndogo wakati anajua kuna maduka zaidi ya 400 ya wafanyabiashara wamewekeza mamilioni yao,"

"Mama kutengua uteuzi wa Mongela amefanya kazi kubwa ya kuponya mioyo ya wafanyabiashara iliyojeruhiwa na Mongela na tumesikia madiwani wameahidiwa kila mmoja kupewa maduka ili wapitishe uwekezaji unaotarajiwa kufanywa eneo hilo la stendi  ndogo "Alisema Mollel.

Usiku wa kuamkia leo Rais Samia alifanya mabadiliko kadhaa ikiweno kuteua ,Kuhamisha na kutengua kwa baadhi ya wasaidizi wake na miongoni mwa viongozi waliopitiwa na mabadiliko.hayo ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Ends....


Post a Comment

0 Comments