TAZAMA MFANYABIASHARA ALIVYOJIMIMINIA SUMU NA KUFA KITUO CHA POLISI ,ALIITWA DAWATI LA JINSIA NA ALIPOONA ANAKANDAMIZWA AKAAMUA AJIMALIZA,RPC AONGEA KILA KITU

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

MCHIMBAJI wa Madini, Gamalieli Munisi Chinga(48)Mkazi wa Muriet amejiua Kwa kunywa sumu mbele ya kituo cha polisi wakati alipoitwa kwenye dawati la jinsia kituo cha  Murieth,Halmashauri ya jiji la Arusha .

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa marehemu Chinga alikunywa sumu  Machi 20 mwaka huu,na kuanguka katika viwanja vya polisi na baadaye kuwahishwa hospitali ya Muriet kuokoa maisha yake, lakini  kesho yake alifariki dunia .

Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda Masejo anasema marehemu alikuwa na mgogoro wa muda mrefu na Mkewe lakini siku hiyo aliitwa polisi katika dawati la kijinsia kwa ajili ya usuluhishi na alipofika katika viunga vya kituo cha  polisi alianguka chini  .

Hata hivyo taarifa zingine zimedai kuwa Marehemu baada ya kufika kituo cha polisi walianza mahojiano lakini hakuridhika na namna alivyokuwa akishurutishwa na askari waliokuwa wakimhoji  jambo ambalo alitishia kunywa sumu.

"Akiwa katika mahojiano alikerwa na hatua ya kushambuliwa na askari waliokuwa kwenye dawati na kutishia kunywa sumu ndipo mmoja ya askari hao alimwambia kuwa usitutishie kama unataka kunywa sumu nenda kanywe ndipo jamaa alitoka kwa hasira na kutoa kitu mfukoni na kubugia mdomoni na baadaye alianguka"alisema mtoa taarifa kituoni hapo.

Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa wa Field Force  Veronica Guta alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema hakuwahi kushuhudia mgogoro huo kati yake na mkewe ila amekuwa akisikia.

Alisema siku ya tulio wawili hao waliitwa kituo cha polisi Murieth, Dawati la kijinsia kwa ajili ya usuluhishi lakini hakuna aliyejua kuwa marehemu aliambatana na sumu mfukoni.

Munisi tayari amezikwa kwao mkoani Kilimanjaro .

Ends. ..








.




Post a Comment

0 Comments