Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Kikundi cha kijamii cha Friends of Batuli cha Jijini Arusha, kimetoa msaada wa vitu mbalimbali vy3nye thamani ya sh,laki 6 kwa shule maalumu ya sekondari Patandi iliyopo Tengeru wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha ili kuwasaidia watoto wenye ulemavu na kuwapatia faraja kutokana na changamoto zinazowakabili.
Akikabidhi msaada huo kwa mkuu wa shule hiyo,Janet Mollel msemaji wa kundi hilo Mwalimu Batuli Kisaya alisema msaada huo wenye thamani ya sh laki 6 ni pamoja na Urine bag PC 30, urine condom za ml.25. PC 30 ,Pumpers medium size box 5
,Urine bag na urine condom za larger size peace 2
,Clean gloves box 2 na
Flagy Paket 4 (dozen 1by10)
Vingine ni Clitrimozole Cream za fungus tube 20
,Deltal liguid soap Lita 2
,Disposable cup PC 4(1by 50)
,Gauze bandage dozen 10
,Themos kubwa
,Gauze roller kubwa
,Godoro dogo Moja ft 2.5 na
Wipes Packet 5.
Alisema kikundi hicho kimekuwa na wajibu wa kuisaidia jamii hususani watoto wenye ujitaji kupitia michango yao kidogo wanaochangishana kwa lengo kuikwamua jamii hiyo na changamoto.
"Leo tumepata fursa ya kufika kwenye shule hii jumuishi na walemavu kwa watoto,tumejifunza na kujionea hali hà lisi ya maisha ya wanafunzi wanaosoma hapa,tumefarijika kuona shule nzuri ambayo inasaidia watoto wenye ulemavu .
Mwl.Batuli aliwashauri wazazi na jamii kwa ujumla kutowaficha ndani watoto wenye ulemavu badala yake wawaibue na kuwaleta katika shule hii maalumu kwa lengo la kuendeleza vipaji vyao .
Alimpongeza rais Samia Suluhu Hasani kwa kutambua makundi maalumu na kuzipa kipaumbele shule maalumu ili kuwapatia elimu makundi maalumu yenye ulemevu wa viungo.
Awali mkuu wa shule ya sekondati Patandi Maalumu Janeth Mollel alishukuru kwa msaada huo uliotolewa na kundi la marafiki la Batuli na kuitaka jamii nyingie na wadau mbalimbali kujitokez kusaidia jamii hiyo yenye ulemavu ilu kuondokana na shid .
Mollel alisema kuwa shule ya Patandi maalumu ni shule ya mfano ilianzishwa mwaka 2021 kwa lengo la kuwaendeleza watoto wenye ulemavu .
Alitoa rai kwa wazazi kuwapeleka watoto wenye ulemavu katika shule hiyo ili kuwaendeleza na kupata elimu bora kama ambavyo watoto wengine wanaosomeshwa na wazazi wao. .
Mmoja ya wanakikundi wa Friends of Batuli, Glori Kaaya alisema wamekuwa wakijitoa kwa michango kidogo kuisaidia jamii yenye uhitaji na wanajisikia faraja kuona makundi maalumu yakiwa na maisha bora kama watu wengine.
Ends..
0 Comments