Na Joseph Ngilisho Arusha
Nchi ya Somalia imekuwa mwanachama Rasmi wa nane wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyokuwa vinahitajika na kuelezwa kuwa itasaidia suala Zima la msukumo wa changamoto za ajira kwa Nchi wanachama pamoja na kupanua soko la pamoja .
Novemba 24,2023 wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki waliridhia Somalia kuwa mwanachama mpya wa jumuiya hiyo inayofikisha sasa idadi ya nchi nane wanachama
Akiongea na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt.Peter Mathuki katika sherehe fupi ya kupandisha bendera na kupokea hati za unachama wa Somalia makao makuu ya EAC Jijini Arusha amesema soka la Jumuiya limepanua wigo na kuwa na watu takribani milioni 350 kwa Sasa na hivyo kuiwezesha jumuiya hiyo kujipanua kibiashara.
Somalia inakuwa mwanachama wa nane wa EAC baada ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania, Rwanda na Uganda.
Hatua hiyo inanuiwa kuimarisha ukuaji wa uchumi nchini humo, ambao bado unaendelea kuimarika kutokana na miongo mitatu ya vita.
Aidha alisema kiwango cha ukuaji wa pato la EAC limeongezeka kutoka Dolla bilioni 2.5 Hadi Dola bilioni 3 na kuongeza soko la ajira kuondoa changamoto za ukosefu wa ajira kwa nchi wanachama na ongezeko la bidhaa kwa kuwa na watu milioni 350 kwa sasa.
Akiongelea suala la usalama Dkt.Mathuki amesema kuwa kuongezeka kwa soka hilo la watu wanaofikia milioni 350 kutaondoa changamoto za upungufu wa ajira na kupelekea wananchi kuchangamkia uzalishaji wa bidhaa na kuuza katika soko la pamoja.
"Hii ni Moja ya kuondoa changamoto za ajira na kurudisha Hali ya usalama katika mataifa ya Jumuiya ikiwa soko la Jumuiya kwa Sasa Lina watu takribani milioni 350 uzalishaji wa bidhaa utaondoa upungufu na kuzalisha ajira hivyo kuwepo kwa usalama katika nchi zetu"
Kwa Upande wake Waziri wa Habari wa Somalia Daud Aweso amesema wanayofuraha Kubwa kukamilisha safari ndef⁰mu ya miaka 12 na safari hiyo ilikuwa na Kazi Kubwa ya changamoto lakini hawakuchoka kufikia hatua hiyo ya kukamilisha utaratibu wa mwisho wa kujiunga na EAC.
Alisema Jumuiya hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa Somalia na nchi zote wanachama kwa kuwa nchi ya nane kujiunga na Jumuiya hii na tunaleta mchango Mkubwa tutakaotoa kuleta maendeleo ndani ya nchi zetu katika uchumi biashara n.k.
Awali Waziri wa viwanda na biashara wa Somalia,Jibril Abdirashid Haji Abdi amesema wanaendelea na wanayofuraha kuwa sehemu ya nchi nane za Jumuiya hiyo ya EAC na wanashukuru kwa kukaribishwa Rasmi na kuahidi kushirikiana na nchi zengine za Jumuiya hiyo kukuza uchumi.
Ends...
0 Comments