Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Arusha,Thomas Sabaya amesema maandamano ya Amani yaliyofanywa na chama cha demokrasia na Maendeleo Chadema ni uchafu na kueleza kuwa serikali haiwezi kuwaletea maendeleo watu watakaojiunga na upinzani.
Sabaya ambaye ni baba yake na Lengai ole Sabaya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, ameibua sintofahamu kwa wananchi huku wakitafsili kwamba kauli hiyo inaweza kuibua migogoro ya kisiasa ambayo ilitulia katika jiji la Arusha na kufanya jiji hilo kutokalika na hivyo kuathiri uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla .
Akiongea na viongozi wa ccm wilayani Longido, Sabaya alikerwa na maandamano hayo akihoji kwanini watu walitoka Longido ,Arumeru na wengine kutoka Moshi kwenda Arusha mjini kuandamana.
"Kwanini msishangae watu wanafanya maandamano wapinzani wapo Moshi Kilimanjaro ,lakini maandamano hayafanyiki Moshi hata siku moja, kwanini yanafanyika hapa ,watu wanaletwa na magari kutoka Rombo,Tanga kwa nini vurugu hii mnatafutiwa ,kwanini msikatae uchafu huo "
"Watu wameletwa kwenye maandamano kwanini tuje kufanya maandamano hapa kwetu ambapo ndipo mahala pametulia kwa maana ya utalii hatua mgogoro ,kwanini mkubali uchafu huo"
"Na sisi tutakaa hivi hivi na chama chetu na wale watakaoenda pembeni kitongoji hicho tuone nani atakayewaletea maendeleo eti mkuu wa mkoa utawapelekea maendeleo???",'mnawapelekea wapinzani maji ya nini ili iwe nini'alisisitiza sabaya Kwa lugha ya Kimasai.
0 Comments