MAHAKAMA YA RUFAA YATUPA RUFAA YA ASKOFU MONABAN,YATHIBITISHA ALIVAMIA ENEO LA MAREHEMU,ATAKIWA KUONDOKA NA KUKABIDHI KWA FAMILIA YA MAREHEMU TITUS, WAKILI WAKE ADAI HIYO NI MAAMUZI YA MWISHO

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Mahakama ya rufaa kanda ya Dar es salaam chini ya majaji watatu leo imetupa shauri la rufaa namba 407/2021 lililofunguliwa na Mfanyabiashara Maarufu,Askofu, wa Kanisa la KKAM, Philemon Mollel akipinga hukumu iliyompa ushindi William Titus Mollel katika mgogoro wa kugombea eneo lililopo Ngulelo nje kidogo ya jiji la Arusha.


Katika hukumu hiyo iliyosomwa  kwa njia ya mtandao na msajili wa mahakama hiyo jijini Dar es salaam, mahakama, imekubali pasipo na shaka  maamuzi yaliyotolewa na mahakama kuu Arusha ,Mei 7,2021 na Jaji Mosses Mzuna yaliyompa ushindi mlalamikaji William Titus Mollel na mwenzake Aron Titus Mollel kwamba mlalamikaji alivamia eneo hilo na hivyo kutupa rufaa hiyo.


Majaji waliosikiliza shauri hilo ni, jaji Lugano Mwandambo ,jaji Paul Kihwelo na jaji Leila Edith Mgonya ambao walisikiliza shauri hilo,Februari 9,mwaka huu , huku upande wa mrufani akiwakilishwa na wakili  Francis Stolla na upande wa mrufaniwa ukiwakilishwa na wakili Mosses Mahuna na Endrew Mganga.


Mahakama hiyo baada ya kupitia hoja za pande mbili imeridhika na uamuzi wa mahakama kuu kanda ya Arusha na kumwamuru mrufani( Monaban) kuondoka katika eneo hilo na kurejesha gharama za mrufaniwa katika shauri hilo .

Wakili Nguli,Mosses Mahuna

Akiongea baada ya hukumu hiyo wakili wa utetezi,Endrew Maganga alisema kimsingi mahakama imetenda haki baada ya kujiridhisha kwamba Monaban alivamia eneo hilo na kujimilikisha na kuendesha shughuli za kijipatia kipato kinyume cha sheria.

Wakili Maganga

Alisema kimsingi mahakama hiyo ndio mahakama ya mwisho katika shauri hilo na kwamba Machi 18 mwaka huu wamejipanga kukaza hukumu na kuiomba mahakama itoe oda kwa dalali wa mahakama  aweze kukabidhi eneo hilo kwa walalamikaji ambao ni wasimamizi wa mirathi .


Naye ,William Titus Mollel (Baraka) alisema Mahakama imetenda haki na wao kama familia wamepokea ushindi huo kwa furaha kwa sababu waliteseka na kesi hiyo kwa muda mrefu wa miaka 8 wakipigania eneo la marehemu baba yao lililokuwa limeporwa .

William TiTus Mollel(BARAKA

Mfanyabiashara askofu,Monaban alipohojiwa alisema bado hajapata hukumu hiyo na anaamini eneo hilo ni mali yake alilinunua kihalali .



Kwa upande wa wakili wa mrufani,Francis Stolla alisema anaheshimu  maamuzi yaliyotolewa na mahakama ila ataangalia namna ya  kumshauri mteja wake kuomba mapitio ya hukumu  hiyo.


Katika eneo hilo Monabani aliendeleza eneo hilo kwa kujenga miradi mbalimbali ikiwemo  kituo cha mafuta , maduka na eneo la kuoshea magari pia hivi karibuni alijenga kanisa kubwa  la KKAM na  hivi karibuni alisimikwa kuwa askofu  .




Mei 7,2021 mahakama kuu kanda ya Arusha ilimpa ushindi William Titus Mollel na mwenzake  Aron Titus Mollel lakini Monaban alipinga hukumu hiyo mahakama ya rufaa.




Ends...














Post a Comment

0 Comments