KANISA LA KKAM LAIBOMOA KKKT ARUSHA, WACHUNGAJI 32 WATIMKA ,WENGINE 20 MWEZI UJAO KUJIUNGA, MAASKOFU KKAM WAKUTANA NA RAIS MWINYI IKULU, UJUMBE MZITO WALIOTETA HUU HAPA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA


Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki KKAM, limeendalea kulibomoa kanisa la kiinjili Kilutheri Tanzania KKKT Mkoa wa Arusha baada ya mchungaji mwingine kujiunga na kanisa hilo na kufikia wachungaji zaidi ya 30 waliojiunga katika kipindi kifupi .

Askofu wa kanisa hilo jimbo la Arusha, Philemon Mollel amebainisha hayo katika ibada ya kumbariki na kumpa wadhifa wa uchungaji ,mwinjilisti Emanuel Zakayo ambaye kwa miaka mingi alihudumu katika kanisa la KKKT.

"Tukio hili limefanyika kwa ufanisi mkubwa likiongeza idadi ya wachungaji wetu na kufikia 32, tunamshukuru mungu kwa kuona kanisa kinavyokua na kuimarika, naimani kwa miaka michache ijayo tutaweza kusimama na kufanya mambo makubwa,endeleeni kutuombea"

Askofu Mollel alisema ujio wa wachungaji hao ni ishara ya kukua na kukubalika  kwa kanisa hilo linaloonekana kama ni geni kwa ukanda huo .


"Kufikia mwezi ujao wa nne tunatarajia kupokea wainjilisti wengine  zaidi ya 20 wakitokea KKKT na sisi hatuna hiyana  tutawabariki na kila mchungaji tunayembariki naimani atakuwa na eneo jipya la kuhudumu maana atakuwa na kundi la watu nyuma yake kwa lengo la kupanua  uinjilishaji"

Akizungumzia ziara yao waliotembelea Ikulu ya  Zanzibar na kukutana na rais Husein Mwinyi ,Askofu Mollel alisema lengo la ziara hiyo ni kufikisha ujumbe wa kiroho hasa ukizingatia kwamba taifa linaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Askofu Mollel na mwenzake Askofu Philemon Mollel (Monaban) Februari 28,mwaka huu,walitembelea Ikulu ya Zanzibar na kufanya mazungumzo na Rais Mwinyi ,mazungumzo ambayo alidai yanalenga kuimarisha imani za kiroho visiwani humo.

Kwa upande wake mchungaji Emanuel Zakayo alisema amefarijika kubarikiwa nakujiunga katika kanisa hilo la KKAM, akidai amezaliwa upya kwani ndoto yale ni kuendelea kuwatumikia watu.

"Nimefurahi kupokea uchungaji kwa mara ya pili,ninatiwa moyo naona ni heshima kubwa mungu ameniheshimu ,na watu wengi walitamani kuona heshima hii lakini haikutokea kwao,lakini nimeinuliwa tena nimezaliwa upya"








Ends...









Post a Comment

0 Comments