INASIKITISHA TAZAMA PICHA, KIFO CHA DEREVA TOURS,MAMA MZAZI AZIMIA KWA KILIO BAADA YA KUONA TUNDU KICHWANI KWA MAREHEMU MWANAYE 'RAIS SAMIA TUSAIDIE' ,NDUGU WATAKA POLISI WANAODAIWA KUMUUA WAWAJIBISHWE,RPC ARUSHA BADO YUPO KIMYA SIMU SIMU HAIPOKELEWI

 Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Vilio na Majonzi vimetawala katika Chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospitali ya Rufaa Mount Meru Mkoani hapa, wakati ndugu jamaa na marafiki wakiaga mwili wa dereva wa utalii,Omari Msamo (48)Mkazi wa Philps Arusha,anayedaiwa kuuawa kwa kipigo cha askari polisi wilayani Karatu.

MAREHEMU OMARI

Tukio la kuuawa kwa Msamo limetokea Machi 16,mwaka huu,katika eneo la Kibaoni Karatu ,baada ya kusimamishwa na askari polisi katika kizuizi cha Manyara Kibaoni,wilayani Karatu na kutokea kutoelewana.

Mama mzazi wa marehemu, Janath Kamugisha alimwomba rais Samia Suluhu Hasani kuingilia kati tukio hilo akidai mtoto wake ameuawa kwa kupigp cha polisi na  kifo chake sio cha kawaida.

Mama huyo alilia kwa nguvu pale alipoona jeraha kubwa la marehemu Kisogoni na kuishiwa kauli nankulazimika kupepewa, wakati akiaga mwili wa mwanaye na kuitaka serikali kuingilia kati huku akilaani wote waliohusika na kifo cha mwanaye.

"Mwanagu ameuawa kikatili rais Samia upo wapi nisaidie unajua uchungu wa mwana, ameniachia watoto wadogo nani atawalea, tunataka serikali iwalee ,hawa waliomuua bado hawajakamatwa nisaidie Rais Samia"

Naye kaka wa Marehemu,Hamidu Maftaa ,alisema marehemu mdogo wake, alikuwa dereva wa kampuni binafsi ya utalii na kwamba siku ya tukio alisimamishwa na askari hao na kushindwa kuelewana.


Alisema askari hao baada ya kushindwa kuelewana na marehemu waliamua kuendesha gari aliyokuwa akitumia na kumpakia hadi kituo cha polisi na baadaye hospitali ya wilaya .

"Haikuweza kufahamika kama Marehemu alifikwa na mauti akiwa eneo la tukio ,njiani ama hospitalini"

Hata hivyo ndugu hao wamesèma wanataka haki itendeke ili ukweli wa tukio hilo uweze kujulikana na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Ndugu hao wa marehemu wamedai kumtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justin Masejo ili kupata ufafanuzi kilichotokea hadi ndugu yao kupoteza maisha lakini hakuweza kupatikana licha ya kumpigia simu yake ya mkononi mara kadhaa lakini ilikuwa haipokelewi

Marehemu ameacha mjane na watoto watatu na anatarajiwa kuzikwa leo Kibolironi ,Moshi Mkoani Kilimanjaro. 














Post a Comment

0 Comments