Na Joseph Ngilisho, Ngorongoro
Wananchi wilaya ya Ngorongoro wamelalamikia hatua ya kupigwa kunakofanywa na watu waliodai ni askari wa jeshi la wananchi Tanzania( JWTZ) ambao wanadaiwa kushiriki kukusanya mapato ya halmashauri kwenye Masoko.
Wakiongea kwa nyakati tofauti walidai kuwa wanajeshi hao wanafanya kazi hiyo ikiwa ni mpango mkakati wa wilaya hiyo kuongeza mapato ya halimashauri hiyo unaofanywa na Mkuu wa wilaya hiyo kanali Willson Sakullo.
Walidai kwamba askari hao wa JWTZ wamepangwa kukusanya ushuru wakiwa wameambatana na maofisa wa Halmashauri kwenye minada ya halimashauri hiyo likiwemo Soko la Posimolu upande wa Kenya na soko la Loika upande wa Tanzania .
Mmoja ya wananchi hao Paulo Sikirai Mkazi wa Kata ya Oloipiri ambaye alikumbwa na masahibu wa kipigwa alidai kuwa askari hao wa jeshi wamekuwa wakiwapiga wananchi pindi wanapopita katika kizuizi cha Posimolu kuelekea soko Loika kupeleka mifugo yao.
"Ukifika kwenye Boda ya Kenya katika soko la Posimolu ili uvuke kueleka soko la Loika upande wa Tanzania ukiwa na mbuzi wawili au hakuna unapigwa ili useme mifugo wengine wapo wapi ili waikamate uweze kulipa ushuru"
Alisema yeye ni mwathirika wa tukio la kipigo ambapo wanajeshi hao wanawatumia wamasai wenzao kuonyesha watu wenye mifuko na kuanza kuwapiga kwa marungu na fimbo.
Naye diwani wa kata Ololosokwani,Moloimet Saing'eu alisema kuwa mpango wa kutumia jeshi la wananchi kukusanya mapato ni mkakati wa mkuu huyo wa wilaya kuhalikisha halmashauri hiyo inapandisha mapato ikiwemo kukabiliana na udanganyifu.
"Wanajeshi wamekuwa wakiambatana na watu wa halmashauri ila wao sio wanaopokea pesa ila wanajeshi wao ni kuwashurutisha wananchi na hivi sasa kunahofu kubwa kwa wananchi na wengine wameacha kuuza mifugo kwenye masoko kwa kuogopa kupigwa na wanajeshi"
Alisema tangu wanajeshi wameingia kusimamia mapato ya halimashauri kwenye masoko na minada, soko la Loika lililopo karibu na Kenya mapato yamepanda kutoka sh,laki nane hadi sh,milioni 1 kwa siku.
Alisema katika mnada wa Kiyaya pia mapato yameongezeka kutoka sh,milioni 1.2 hadi milioni 5.5.Diwani alikiri kuwepo matukio ya wananchi kupigwa hasa kwa wale wanaofanya udanganyifu wakati wa kuingia kwenye minada .
"Ni kweli watu wanapigwa unajua hivi sasa kuingia kwenye mnada wowote halmashauri imeweka utaratibu kila anayeingia lazima atozwe kiingilio hata kama hana mfugo wowote ,hii ni kuwabana wale wanaodanga kuwa hawana mifugo ya kuuza wati wanapitisha kinuemela na sasa hivi ushuru wa mifugo umepanda kutoka sh, elfu 7 hadi sh, 35 kwa ng'ombe mmoja"
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Njoroi ulipo mnada wa Olaika,James Taki,alisema ni kweli wanajeshi ndio wanaotumika kukusanya mapato katika soko hilo ambalo linatumiwa na wafanyabiashara wengi wa mifugo wanapovuka kuelekea nchini Kenya.
"Sisi kama viongozi hatushirikishwi zoezi la ukusanyaji WA mapato ya halmaahauri, tumeshtulia tu tunawaona wanajeshi kwenye masoko wakikusanya ushuru,jambo hili limewashtua sana jamii ya WAMASAI si unajua walivyo waoga"
Alisema kuwa WANANCHI wamekuwa wakitozwa gharama kubwa za kulipia ushuru wa mifugo kwa kulipia sh,32000 kwa kila kichwa cha Ng'ombe na sh, 8000 kwa Kondoo na mbuzi
Hata hivyo alisema hajapata malalamiko ya wananchi wake kupigwa kwa kuwa wao kama viongozi hawashirikishwi wakati zoezi la kukusanya mapato likifanyika.
"Nikweli wanajeshi ndio wanaokusanya mapato ila suala la watu kupigwa nimekuwa nikisikia ila sijapata malalamiko rasimi"
Alisema pamoja na kwamba yeye ndiye alishiriki ujenzi wa miundo mbinu katika soko hilo ila huwa hashirikishwi shughuli za ukusanyaji wa mapato siku za soko.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri, Emanuel Sukumus alipohojiwa kwa njia ya simu alishindwa kukubali ama kukanusha alisema jambo hilo wameambiwa wasilizungumze ila kwa idhini ya mkuu wa wilaya pekee.
"Hili suala mimi sina mamlaka ya kulizungumza tumeambiwa tusiliseme labda umtafuta mkuu wa wilaya ndo analifahamu zaidi ama mwenyekiti wa halmashauri "
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro,Kanali Wilson Sakullo alipohojiwa juu ya malalamiko hayo , alikanusha jeshi la wananchi Tanzania kutumika ukusanyaji wa mapato ya halmashauri hiyo.
"Sio kazi ya Jeshi kukusanya Mapato ya halimashauri, hizo taarifa hazina ukweli wowote"
Mkuu huyo alikiri kupanda kwa mapato yanayotokana na masoko na Ä·ueleza kuwa hiyo ni mikakati ya wilaya kuhakikisha halmashauri mapato yanapanda"
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Mohamed Bayo alipotafutwa alisema yupo nje ya ofisi hawezi kuzungumza chochote.
Ends..
0 Comments