Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Watu watano wamefariki dunia papo hapo huku wengine 15 wakijeruhiwa, baada ya gari dogo la abiria aina Haice kuligonga lori la magogo lililokuwa limesimama pembezoni mwa barabara ya Arusha Namanga,wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha.
Haice aina ya Nissan Caravan, lenye namba za usajili T 958 DFM, liligonga kwa nyuma lori aina Fiat, lenye namba za usajili T 551 AFP, lililokuwa limebeba magogo kwenye kijiji cha Ekenywa barabara ya Namanga-Arusha wilaya ya Arumeru.
.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, alisema hadi sasa vifo ni watano waliopoteza maisha papohapo na majeruhi kadhaa wapatao 15 na uchunguzi wa ajali hiyo bado unaendelea.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa ajali hiyo imelihusisha gari hilo aina ya Haice linalofanya Safari zake likitokea DonyoSambu kwenda Ngaramtoni na lilipofika eneo la tukio dereva aa haice alishindwa kumudu gari lake na hatimaye kuparamia gari hilo la Magogo.
Ajali hiyo imetokea ikiwa ni wiki tatu kupita tangia ajali nyingine mbaya kuua watu takribani 25 baada ya kuhusisa magari matatu.
Shuhuda wa ajali hiyo, Amija Mollel alisema akiwa amesimama akisubiri usafiri majira ya saa 2.40 usiku jana akisikia kishindo na aliposogea eneo hilo ndipo alipobaini Haice imegonga nyuma ya lori la magogo .
Alisema gari dogo ya abiria lilikuwa linatokea Donyosambu kwenda Ngaramtoni na lilipofika eneo la Ndiogi Mamsa dereva wa Haice ambaye hakujulikana aliligonga kwa nyuma Lori hilo lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara na kusababishwa vifo vya watu waliokuwa kwenye gari dogo.
Kamanda Masejo wa jeshi la polisi Mkoa wa Arusha alisema uchunguzi wa tukio hilo, bado unaendelea na majeruhi wanaendelea vizuri akiwemo dereva wa Haice.
Ends...
0 Comments