Na Joseph Ngilisho -ARUSHA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jana kimehitinisha Maandamano yake ya awamu ya kwanza kwa kishindo yaliyofanyina katika jiji la Arusha licha ya mvua kubwa kunyesha.
Maelfu ya waandamanaji katika jiji la Arusha walijitokeza kuyaunga mkono wakiwemo madereva wa bodaboda ,Bajaj na Watembea kwa miguu wakitembea umbali wa zaidi ya kilometa 50 ikiwa ni jumla ya kilometa 169 walizotembea tangia waanze maandamano hayo katika majiji ya Dar,Mwanza,Mbeya na hatimaye Arusha.
Mwenyekiti wa chama hicho Taifa ,Freeman Mbowe alisema kuwa baada ya kuhitinisha awamu ya kwanza kwa majiji hayo manne wanaenda kutia nanga mkoani Mtwara ili kuona mapokei ya serikali yakoje na baadaye wataibuka na mazimio mapya.
Mbowe alisema ccm imeishiwa pumzi ikiwemo kushindwa kuthibiti wizi wa fedha za umma unaofanywa na baadhi ya watumishi wa umma kupitia miradi ya maendelo.."Asilimia 30 ya matumizi ya fedha za serikali ni wizi mtupu" .
"Maandamano kwa sasa ni Utamaduni wa chadema,ili kufikisha kilio cha wananchi kwa watawala,tumekaa vikao vingi vya maridhiano lakini imekuwa kama danganya toto na baada ya hapo hakuna mafanikio "
Alisema maandamano yao yalilenga mambo mbalimbali ikiwemo maisha duni ya Watanzania wakiituhumu serikali ya CCM ,kupanda kwa bidhaa kama sukari ,mafuta , vyakula na pia kuishinikiza serikali kuridhia kwa vitendo makubaliano ya uwepo wa katiba mpya ,tume huru ya uchaguzi pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu inayoendelea kwa jamii ya maasai kufukuzwa kwenye makazi yao.
Maandamano hayo yalipangwa kwa njia nne kuu na kuhitinishwa katika mkutano mkubwa uliofanyika katika viwanja vya Relini jijini Arusha, ambapo viongozi kadhaa walihutubia akiwemo dkt Willbrod Slaa na wakili Bonface Mwambukusi.
Naye makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu amesema sehemu nyingine duniani Polisi hutaja njia ambako maandamano yatapita na kutoa tahadhari kwa wafanyabiashara pamoja watu wanaotumia barabara hiyo wajue itatumika kwa maandamo, lakini maandamano ya CHADEMA yanafanyika huku magari yanaingilia msafara wao wa maandamano.
Akiongeza, kuchanganya waandamanaji na magari sio sawa kwani maafa yanaweza kutokea, na kuwataka polisi wafanye kazi yao ya kuwasaidia waandamanaji kuandamana kama wanavyofanya kwa Makonda. Akisema Makonda akifanya mikutano yake polisi wanahakikisha barabara inakuwa wazi lakini wakifanya CHADEMA ni tofauti, waandamanaji wanachanganywa na magari.
Awali aliyewahi kuwa mbunge wa Arusha Mjini God bless Lema,aliwashukuru wananchi kwa kwa kujitokez kwa vingi katika maandamo hayo nakusema waandamanaji hawatajutia na kumtaka mbunge wa Arusha Mrisho Gambo kuanza kufungasha mapema.
Ends...
0 Comments