TAZAMA ARUSHA ILIVYOZIZIMA KWA KILIO,WATU WATOKWA MACHOZI NA DAMU KUAAGA MIILI YA VIFO 25,11 NDO WAMEAGWA ,DKT CHANA AONGOZA KUAGA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana ameongoza maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wa Arusha kuaga na kutoa heshima ya mwisho kwa Miili ya Marehemu waliofariki katika ajali mbaya iliyohusisha lori na magari madogo matatu katika eneo la  Ngaramtoni nje kidogo ya jiji la Arusha katika barabara kuu ya Arusha - Namanga








Miili ya Marehemu 11 kati ya 25 waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea Jumamosi iliyopita ndiyo iliyoagwa  huku miili ya marehemu wengine 14 ikiwa imeshachukuliwa na ndugu wa marehemu hao.


Awali Vongozi wa madhehebu mbalimbali wa Dini wametoa maneno ya faraja kwa wafiwa ambao ni Dkt.Stanlet Hotay kwa madhehebu wa Kikristu na Sheikh Hussein Said kwa dini ya Kiislam


Balozi Dkt.Pindi Chana amewasilisha salamu za pole za serikali huku Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella akitoa taarifa za maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuwafariji wafiwa kwa kushiriki kikamilifu katika mazishi


Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Loy Thomas Ole Sabaya amewasilisha salamu za  Katibu Mkuu wa chama hicho Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi.


Ajali hiyo pia imehusisha raia wa kigeni ambapo Kaimu Balozi wa Kenya nchini Nancy Sifa ametoa salamu za pole










Post a Comment

0 Comments