Na Joseph Ngilisho Arusha
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Arusha inamshikilia mfanyabiashara maarufu anayemiliki vituo vya mafuta jiji la Arusha, Maganga Baha lago akituhumiwa kujifanya afisa Misitu na kuomba rushwa ya shilingi 100,000.
Kamanda wa Takukuru Mkoa, Zawadi Ngajilo amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kudai kwamba uchunguzi wa tukio unaendelea kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
"Ni kweli huyo mfanyabiashara amekamatwa na sasa tupo kwenye hatua ya uchunguzi na tukikamilisha tutawapatia taarifa za tukio hilo"
Taarifa zimedai kwamba mtuhumiwa alikamatwa katika kituo chake cha Mafuta kilichopo eneo la Morombo baada ya kuwekewa mtego na kukutwa na kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mmoja ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya kusafirisha mkaa bila kufuata sheria kutoka wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara na kuleta jijini Arusha.
Imeelezwa kwamba Maganga akishirikiana na wenzake anatuhumiwa kuwatisha watu wanaoendesha biashara hiyo ya zao la misitu kwa kuwaambia kuwa yeye ni afisa misitu na baadaye akiwa na wenzake hukamata mali zao na kuwapeleka kwenye kituo chake cha mafuta ambako kuna eneo la maficho na kuomba rushwa ili wasiwapeleke kwenye vyombo vya sheria wakiwatisha kuwafungulia kesi ya uhujumu uchumi.
Hata hivyo mmoja ya maofisa wa Takukuru aliyehusika kumkamata mtuhumiwa huyo(jina linahifadhiwa) , alidai kwamba mtuhumiwa aliwaambia ametumwa na mkuu wa wilaya ya Arusha, Jambo ambalo DC alipoulizwa aliruka futi 100 na kuiagiza takukuru ichukue hatua zote za kisheria dhidi yake.
"Mimi ndio nimeagiza wamshikilie na akae lokapu na taratibu zote za kisheria zifuatwe ,siko hapa kushirikiana na mhalifu uoyote" alisema DC Ofisini kwake
Akiongelea tuhuma hizo baada ya kuachiwa kwa dhamana Maganga alikiri kukamatwa na takukuru na kuwekwa mahabusu ila alisema sio yeye aliyehusika na mpango huo na kudai alikuwa akimsaidia kumwomba mhusika aliyekamatwa apunguziwe bei badala ya kulipa sh, laki nne alipe sh, laki moja ambayo ndio walikubaliana.
Ends....
.
0 Comments