Na Joseph Ngilisho- ARUSHA
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya amewaomba msamaha watanzania wote wanaohisi kwamba aliwakosea huku akisisitiza kuwasamehe wale wote waliomkosea
Aidha Sabaya alimshukuru rais Samia Suluhu Hasani kwa kuweka mfumo wezeshi wa kimahakama uliosaidia upatikanaji wa haki na kupunguza msongamato wa mahabusu na wafungwa magerezani
Sabaya amesema hayo leo katika Kanisa la Ebenezer Restoration Ministry for All Nations, lililopo Moshono jijini Arusha, wakati alipohudhulia ibada ya kumshukuru Mungu baada ya kumaliza changamoto zilizokuwa zikimkabili.
Akiwa ameambatana na mke wake Jesca Nasary pamoja na waliokuwa washtakiwa wenzake ,alitangaza mbele ya kanisa hilo kwamba hatanyanyua mkono wake kupigana na wale wanaoendeleza chuki dhidi yake, ila ataacha madhabahu ya mungu ipigane nao.
"Leo naomba nitangaze mbele ya madhabahu hii kuwa kama kuna mtu nimemkosea namwomba anisamehe na kama ataendelea na vita naiachia madhabahu hii ya mungu ipigane naye namshikuru sana rais Samia na wote walioniombea na sasa nipo huru"
Alisema alihukumiwa kufungwa miaka isiyopungua 90 na watu walisema maneno mengi ila anamshukuru mungu aliyekuwa amemtanguliza mbele kwa kumwomba usiku na mchana na hatimaye ameyashinda majaribu.
"Kama si mungu kutumika kupitia rais Samia nchi isingekuwa hapa, nimeingia jela June 2,2021 nimekuta mahabusu zaidi ya 4000 lakini hadi natoka nimeacha mahabusu 180 hizo no jitihada kubwa za rais wetu samia"
"Nimekutana na Mungu uso kwa uso nikiwa jela na ndiye aliyenitendea makuu na sasa nipo huru"
Naye mchungaji Mosses Kaaya aliyekuwa mahabusu gereza kuu la Arusha, alisema kuwa Sabaya kwenda jela ilikuwa ni kusudio la mungu kwani akiwa jela alishuhudia Sabaya akiwasaidia watu wengi kuwaandikia rufaa ambao walifungwa kimakosa na kufanikiwa kushinda rufaa zao.
"Sabaya alienda jela kwa kusudio la mungu kwani watu wengi amewasaidia kutoka jela kwa kuwaandikia rufaa, tunamshukuru sana rais Samia kwa kupunguza mrundikano wa wafungwa na mahabusu kwenye magereza "
Naye mama yake na Sabaya, Vida Sabaya alimshukuru mungu kwa kuyashinda majaribu kwa mwanaye kwani alidai kupitia mapito magumu wakati wa sakata la sabaya huku watu wengi wakimkatisha tamaa kuwa mtoto wake hatatoboa ila ni wa kuozea jela.
"Sijawahi kupita kwenye mapito magumu kama haya ila namshukuru mungu ametenda"
Kwa upande wake mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo la Ebenezer Restoration Ministry for All Nations, Frederick Kalinga,alimpongeza sabaya kwa uamuzi wa kumshukuru mungu baada ya kumtendea miujiza na kuitaka jamii kuwa na desturi hiyo.
Mch Kalinga ambaye aliongoza ibada hiyo ya shukrani alimtabiria Sabaya kuwa mtu Mashuhuri hapa nchini na hivi karibuni atapata uteuzi muhimu kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
Naye askofu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM),Philemon Lenges Mollel alimtaka Sabaya kukamatana na yesu kwani ni yeye pekee mwenye uwezo wa kumwinua.
Alisema uwepo wa Ibada hiyo ya shukrani sio kwa ajili ya kumsafisha Sabaya ila wapo hapo kwa ajili ya kumshukuru mungu.
"Tumefika hapa kukshukuru mungu na sio kumsafisha Sabaya na tunachoweza kusema bi kumwomba ashikamane na yesu ambaye ndio mwenye uwezo wa kumwinua"
Katika ibada hiyo ya kumshukuru mungu Sabaya tangulia aliposhinda kesi mbili na nyingine kuachiwa huru hakuwahi kuzungumza hadharani hadi leo hii alipoibukia kanisani.
Sabaya aliwasili kanisani hapo akiwa ameongozana na mke wake Jesca Nasary, Ndugu, Jamaa na marafiki viongozi mbali mbali wa chama na serikali.
Wengine waliomsindikiza katika ibada hiyo ni pamoja na mawakili waliomsimamia kesi zake ,madiwani wa Halmashauri ya Arusha ,Mkurugenzi mstaafu wa Wilaya ya Hai pamoja na katibu tawala wa wilaya hiyo na makada wa ccm kutoka Hai na kupelekea kanisa hilo kufurika mamia ya watu wakimlaki Sabaya .
Ends....
.
0 Comments