Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inaendelea kutoa kipaumbele kwa wanaosoma masomo ya Sayansi ikiwemo kutoa ufadhili wa masomo ili kuongeza hamasa kwa Vijana wa kitanzania wakiwemo wasichana kupenda kusoma masomo hayo.
Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Februari 11, 2024 mkoani Arusha katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi, ambapo amesisitiza kuwa serikali pia itaendelea kuwekeza katika mazingira mazuri kwa ajili ya Vijana kupata fursa mbalimbali katika nyanja za Sayansi za masomo na kuendeleza ubunifu ili kuendana na kasi ya teknolojia duniani na hata soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Mkenda alisema kuwa wanawake na wasichana ni watu muhimu kwa mustakabali wa Sayansi na kumpongeza Mkurugenzi wa shule ya Sayansi Frof Nuhu Hatibu akidai ni gwiji aliyebobea katika elimu hiyo na kusema kuwa anastasia sifa na kuigwa .
Hata hivyo alisema Fursa za kazi duniani zinategemea elimu ya TEHAMA tusipoweza kuwafundisha vijana wetu katika eneo la sayansi tunawanyima fursa za ajira " Wizara ya elimu imejipanga vizuri kuendelea kutekeleza ufadhili kwa wahitaji wotee na sisi wote na wadau wa elimu tutakuza sayansi hapa nchini natutafanya kila liwezekanalo wasichana wengi kusoma masomo ya sayansi ilikukuza uchumi wetu".alisema
Akiongea kwa niaba ya wadau wa Elimu Prof. NUHU HATIBU kutoka chuo Cha sayansi Arusha amesema ni muhimu Kuhusisha elimu ya ubunifu na ajira ili kuweza kuwapa vijana wa kitanzania fursa katika miradi mbalimbali itakayofanywa nchini .
Elimu Bora ni elimu ya ububifu na ajira ambayo itasaidia kuondoa changamoto kubwa sana ya upatikanaji wa ajira Tanzania.
"Inasikitisha sana mwaka huu tunasherhekea miaka 51 tangu kuanzishwa kwa mechanical engineering na hatuna mainjia wakujenga nchi tunaiomba serikali kupitisha sheria inayosema miradi yote ya miundombinu katika ganzi ya mkoa isipitie nje ya nchi kwasababu ili kutoa hamasa yakujifunza sayansi na teknolojia ni lazima tuunganishe na ajira kwa vijana wote wanaohitimu masomo hayo ya sayansi."alisema Profesa Hatibu
Endssss
0 Comments