Joseph Ngilisho ARUSHA
Aidha ametumia fursa hiyo kuwapongeza kwa namna walivyoendelea kudhibiti ajali kipindi cha mwisho wa mwaka na mwanzoni mwa mwaka 2024 huku akiwataka kuendelea kutoa elimu ya namna bora ya matumizi ya Barabara ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika .
Kwa upande wake Naibu kamishna wa polisi ambaye ni kamanda wa kikosi Cha usalama barabarani Ramadhani Ng'anzi amesema lengo la mafunzo hayo kwa wakuu wa usalama barabarani na wakaguzi wa magari ni kuwajengea maarifa makubwa zaidi katika fani zao.
Pia Ng'anzi amesema wameweza kutembelea karakana mbalimbali katika chuo Cha ufundi Arusha na wameona jinsi Gani chuo hicho kilivyopiga hatua katika kutoa elimu ya kisasa zaidi hapa nchini.
Naye mkuu wa chuo Cha ufundi Arusha Musa Chacha amesema wamefarijika sana kupata ugeni wa jeshi la polisi upande wa usalama barabarani amesema mashirikiano baina yao na jeshi Hilo yataendelea na watahakikisha Tanzania inakuwa salama pindi wanapotumia vyombo vya moto .
Aidha Chacha ameongeza kuwa wamekuwa wakishirikiana na jeshi la polisi kuandaa mafunzo mbalimbali hapa nchini pamoja na kuwaongezea hujui wataalam wa jeshi la polisi katika ukaguzi wa magari ikiwa ni kuhakikisha wanawaondoa madereva wazembe na wasio na elimu barabarani.
Kwa upande wake Afisa mnadhimu wa kikosi cha Usalama barabarani kamishna msaidizi wa Polisi ACP Pili Misungwi amesema mfumo huo unakwenda kudhibiti madereva wasio na sifa ambapo amewaomba wakuu wa kikosi hicho kuyapokea mafunzo hayo ambayo yanakwenda kumaliza changamoto zilizokuwepo.
Mkuu wa Taasisi ya Mitambo Mizito na Teknolojia Asia Nyuda Ntembo amesema lengo la mfumo huo ni kuvitambua vyuo ambavyo vimesajiliwa ambao amebainisha kuwa waliona changamoto hiyo kitendo kilichopelekea kuungana na Jeshi la Polisi na kuja na mfumo wa Pamoja wa kuvitambua shule za udereva.
Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya Mitambo mizito na Teknolojia IHET naibu kamishna wa Polisi Mstaafu Mohamed Mpinga amesema kuwa hapo awali kulikuwa na changamoto huku akisema taasisi hiyo itasaidia kudhibiti shule za udereva zisizokuwa na sifa hapa nchini.
Ends..
0 Comments