MSIBA WA LOWASA BALAA,LAIGWANANI WACHAFUKWA WATOA NG'OMBE 100 WACHINJWE ,WATU WATAFUNA NYAMA MENO YANAUMA TAZAMA HAPA

Na Joseph Ngilisho MONDULI


Wazee wa kimila almaarufu LAIGWANANI wameamua kumuenzi aliyekuwa waziri Mkuu hayari Edward Lowasa kwa kutoa ngo'mbe wapatao 100 ili watumike kama kitoweo katika msiba huo unaofanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Ngarashe wilayani humo.








Laigwanani Jackson Teteyo kutoka wilaya ya Simanjiro alisema hadi sasa  ng'ombe zaidi ya 40 wameshachinjwa na ng'ombe 57 wanatarajiwa kuchinjwa kwa ajili ya kufanikisha shughuli hiyo ya mazishi inayofanyika nyumbani kwa Marehemu ,Ngarashe wilayani humo.

Alisema idadi ya Ng'ombe hao wanatolewa na wafugaji wenye mapenzi mema na marehemu , wakikumbuka namna marehemu alivyokuwa na desturi ya kuchinja ng'ombe na kuwaalika watu mbalimbali nyumbani kwake.

"Lowasa alikuwa mwanamapinduzi amepambana sana juu ya jamii yake alipambana sana kuhakikisha watoto wa kifugaji wanaenda shule na alijitahidi kutuletea maji ndio maana umeona wamasai wameamua kujitolea ng'ombe kwa ajili ya kumuenzi"

Naye Linganasa Soipey kutoka wilaya ya Simanjiro alisema kifo cha Hayati Lowasa ni pigo kubwa kwa Monduli na jamii yake kwani wananchi wa Monduli walizoea kila mwisho wa mwaka marehemu alichinja ng'ombe wa kutosha na kuwaalika wananchi kwa chakula nyumbani kwake...









ENDS...


Post a Comment

0 Comments