Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Mashirika Matano yasiyokuwa ya kiserikali Mkoani Arusha yatoa tamko zito la kupinga Misheni ya UNESCO kufuatilia eneo la uhifadhi la Ngorongoro yakidai kuwa haliwezi kutoa matokeo huru na haki kwa jamii ya wamasai walioathiriwa na janga hilo.
Aidha wametoa maombi ya pamoja ya kutaka Ngorongoro iondolewe katika eneo la Urithi wa Dunia iwapo usajili wake utashindwa kuendana na ulinzi wa haki za binadamu kwa wakazi wa eneo hilo.
Akisoma tamko hilo kwa niaba ya mashirika hayo Mkurugenzi wa Shirika la CILAO ,Odero Odero alisema mashirika hayo kwa pamoja yanaitaka UNESCO kusitisha Misheni yake ya ufuatiliaji katika eneo la uhifadhi la Ngorongoro ambapo tamko hilo lilidai kutokuwepo na matokeo huru na halali.
"Tunaita UNESCO, IUCN na ICOMOS kusitisha misheni hii ambayo haiwezi kutoa matokeo huru na halali kwani haikuweza kusikia wamiliki wa haki na Jamii za Maasai zilizoathiriwa katika Eneo la Ngorongoro na Msomera"alisema Odero
Alisema Misheni hiyo ya kufuatilia eneo hilo la Ngorongoro ilianza kwa Siri ambapo ilifika nchini Februari 3, 2024 na ilitarajiwa kukamilika Februari 9, 2024 ambapo ilihamasishwa na shinikizo kutokana na kilio Cha wamasai na mashirika ya haki za binadamu na ardhi za wakazi wa Maasai katika vijiji 25 vilivyosajiliwa kihalali.
Katika tamko hilo inadaiwa kuwa Misheni hiyo ilifanya Mkutano katika Ofisi ya kamishna wa mkoa wa Arusha kikiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki na baadaye kukutana na wadau wanaopigania kuhamishwa Kwa nguvu ya Maasai kutoka ardhi Yao ya kiasili Ili kupisha Utalii.
"Serikali imejaribu mara Kwa mara kuwahamisha Maasai kutoka NCA mwaka 2021 ilianza kwa hiari Jamii kutoka eneo hilo kwenda kijiji Cha Msomera .
Alisema Msomera ni kijiji kilichosajiliwa kihalali kilichoishi Kwa kiasi kikubwa na wafugaji wa Maasai katika Wilaya ya Handeni ya mkoa wa Tanga umbali wa kilomita 500 kutoka Ngorongoro, ila Maasai wa Msomera hawakutoa idhini Kwa uhamishaji huu ambao unawafukuza" alisema
Odero aliituhumu serikali kwa uvunjaji wa haki za binadamu na ardhi kwa wananchi wa Ngorongoro .Alisema Februari 6 mwaka huu Zaidi ya madiwani 20 ,wenyeviti wa vijiji na viongozi wa wanawake kutoka Ngorongoro walimwandikia UNESCO na wizara ya Maliasili kueleza kutoridhika kwao na mwenendo wa suala hilo.
Ends.
0 Comments