Na Joseph Ngilisho MONDULI
RAIS Samia Suluhu Hassan ameongoza mazishi ya Hayati Edward Lowassa na kusema kuwa taifa linajivunia yale yaliyofanywa na marehemu enzi za uhai wake akiwa mtumishi wa serikali na yanapaswa kuigwa.
Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati aliposhiriki maziko ya hayati Lowassa yaliyofanyika kijijini kwake Ngarashi wilayani Monduli mkoani Arusha leo na kuhudhuliwa na maelfu ya wananchi wakiwemo viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema inapotajwa historia ya hayati Edward Lowassa lazima kitajwe chama hicho.
“Unawezaje ukaiandika historia ya Lowassa ukasahau utumishi wake wa miaka minne kama Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, kama mgombe wa urais wa mwaka 2015 ambaye aliijenga demokrasia kwa viwango ambayo havijawahi kufikiwa na mgombea yoyote wa upinzani”. amehoji Mbowe.
Mkuu huyo wa nchi amesema Lowassa alipenda vijana wapate ujuzi na maarifa ndio maana alipokuwa mgombea urais mwaka 2015 aliweka wazi kipaumbele chake cha kwanza kuwa ni elimu na pili elimu na cha tatu elimu.
“Lowassa alikuwa muumini wa elimu kama nyenzo ya kujikwamua na umasikini na mara zote alisistiza kwamba haupendi umasikini,”
“Ninakumbuka aliwahi kusema nimekuwa na nitaendelea kusisitiza umuhimu wa elimu bora kwa wote, elimu inayowaandaa vijana kuingia kwenye soko la ajira la dunia”. amesema
Ameongeza kuwa dhamira ya Lowassa ya kutaka kusimamia sekta ya elimu ndio matunda yanayoonekana sasa ya kuimarika kwa sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa la shule nchini.
Miongoni mwa waombolezaji waliohudhulia mazishi hayo, akiwemo katibu wa siasa na uenezi Meru, Kennedy Mpumilwa alisema kuwa amejifunza uthubutu wa Lowasa na uwajibikaji kwa maslahi ya taifa na anastahili kuigwa .
Ends..
0 Comments