By Ngilisho Tv
Antuja Msuya ambaye ni Dada wa Marehemu Bilionea Erasto Msuya ameangua kilio leo baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuwaachia huru Wifi yake ( Miriam Mrita ambaye ni Mke wa Bilionea Msuya) pamoja na Mtu mwingine mmoja ambaye ni Mfanyabiashara aitwae Revocatus Everist.
Mahakama hiyo ilijiridhisha kuwa wawili hao hawahusiki na kifo cha Mdogo wa Erasto Msuya aitwae Aneth Msuya aliyeuawa kwa kuchinjwa Wilayani Kigamboni Mei 26, 2016 jijini Dar es salaam.
Antuja aliangua kilio hicho Mahakamani hapo jioni ya leo na kupaza sauti “ushahidi wote unaonekana Mtu anaambiwa hana hatia, niueni... niueni, niueni, bora nife”
“Hakuna haki iliyotendeka maana ushahidi wote unaonekana na ushahidi upo na jinsi ilivyofanyika mwanzo hadi mwisho ila wameamua maamuzi yao Mahakama haijatenda haki, kuanzia Arusha wanapaka nyumba rangi, upare wanapaki nyumba rangi wanasema anatoka kwa gharama yoyote leo ametoka, Mungu ataamua” - Antuja ameyasema haya mbele ya Waandishi wa habari.
Miriam Mrita
Hata hivyo wakati wakitoka Mahakamani hapo, Ndugu na Jamaa waliofurahishwa na kuachiwa huru kwa wawili hao walisikika wakitamka baadhi ya maneno ya kumshukuru Mungu mbele ya Antuja “Yesu ni bwana, amefanya”
0 Comments