HAKIMU MBARONI KWA KUMLAWITI DEREVA BODABODA,ALIMNYWESHA BOMBE NA KUMLAWITI "ALIPOFUNGUA MLANGO SEHEMU ZAKE ZA SIRI ZILIKUWA JUU

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Loliondo,Benson Ngowi(32) anashikiliwa na jeshi la Polisi katika kituo cha Loliondo,Wasso kwa kosa la kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Wasso wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha .

Hakimu Benson Ngowi anayetuhumiwa kumlawiti DEREVA BODABODA 

Kwa mujibu wa chanzo cha Habari wilayani humo,tukio hilo limetokea jana majira ya saa tatu na saa nne usiku nyumbani kwa kijana huyo ambaye hufanyakazi ya kuendesha pikipiki maarufu bodaboda katika eneo la Wasso.


Mtoa taarifa alifafanua kwamba Hakimu huyo ambaye hivi karibuni alihamia kikazi,alionekana majira ya mchana akiwa na kijana huyo na baadaye jioni walienda kunywa pombe nyumbani kwa kijana huyo ambaye ànaishi chumba kimoja na sebule


Alisema ilipofika majira ya usiku kaka yake na kijana aliyelawitiwa (jina linahifadhiwa) alifika  nyumbani kwa mdogo wake na kumkuta mdogo wake wakiwa na hakimu wakiendelea kunywa pombe aina ya Safari huku hakimu ndiye aliyekuwa akinunua pombe.


Taarifa inasema kkwamba ilipofika majira ya saa tatu usiku Hakimu alimtuma kaka yake na kijana huyo kwenda kuchukua chakula na wakati aliporejea alikuta mlango umefungwa na kuamua kuwagongea


"Baada ya kugonga Hakimu alifungua mlango lakini chaajabu alionekama  sehemu yake ya siri imesimama  ndipo kaka yake alipopatwa na mshtuko
 na kuamua kuingia chumbani kwa mdogo wake  kujua kulikoni  na kumkuta akiwa amelala kitandani kifudifudi akiwa utupu hajitambui"alisema mtoa taarifa


Alisema baada ya kushuhudia tukio hilo aliamua kutoa taarifa kwa watu mbalimbali ndipo na miongoni mwa watu waliofika kushuhudia tukio hilo ni pamoja na hakimu wenzake  na baadaye polisi walitia timu .

"Walimkuta kijana hajitambui kitandani na baada ya kumwamsha na kuzinduka alihisi maumivu sehemu zake za haja kubwa na walipomuuliza alionekana kuduwaa nini kimetokea"


  Askari hao walimtia nguvuni mtuhumiwa, licha ya kwamba aliomba asamehewe akidai ni pombe imempitia.


Kijana huyo alipelekwa katika hospitali ya Wasso kwa matibabu na taarifa ya daktari imeonesha kuwepo na michubuko sehemu za haja kubwa pamoja na mbegu  za kiume.


Taarifa zinadai kwamba mtuhumiwa alikuwa na mazoea na kijana huyo ya kumtuma mara kwa mara ikiwemo kumsafirisha kutoka eneo moja kwenda jingine kwa kutumia pikipiki yake .


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Justin Masejo alipotafutwa alisema bado hajapata taarifa ila anafuatilia tukio hilo na atatoa taarifa.

E ds..












Post a Comment

0 Comments