CEDHA YAENDELEA KUWANO WATAALAMU WA AFYA NCHINI,SERIKALI BILA MBAMBAMBA YAIMWAGIA MABILIONI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE ,MKUU WA CHUO AMWAGIA SIFA RAIS SAMIA

 Na Joseph Ngilisho -ARUSHA 

SERIKALI imetenga kiasi cha shilingi bilioni nne kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa ajili ya uboreshaji wa miundo mbinu ya Taàsisi ya Afya ya CEDHA ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake ambayo ni pamoja na kuandaa walimu bora wa kufundisha vyuo vya Afya nchini .


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela kupitia hotuba yake iliyosomwa na kaimu mganga mkuu wa hospital ya Rufaa Mt Meru dkt Edna Ntulwe wakati akifungua mafunzo ya viongozi wanaosimamia huduma za afya kutoka mikoa mbalimbali nchini, yanayofanyika kwa siku 11 katika chuo cha afya cha CEDHA, jijini Arusha.

Mongela alisisitiza kuwa fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa ili Taasisi hiyo ya CEDHA iweze kufikia malengo yake ya  kuendeleza Taaluma za watumishi wa Afya walio kazini ,kufanya Tafiti za kutatua changamoto za Afya na kutoa ushauri Elekezi kuhusu huduma za Afya.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya ikiwemo ujenzi wa Hospitali,Vituo vya Afya na Zahanati ,ununuzi wa dawa na Vifaa Tiba pamoja na kutoa ajira katika sekta hiyo .

Mongela aliwataka wataalamu wa Afya kujiendeleza kielimu ili kuendana na uwekezaji huo.

Alitoa Rai kwa washiriki wa mafunzo hayo kutoka vituo vya afya vya serikali, binafsi, vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na bandari ya Dar Es Salaam na Tanga ,kuyatumia mafunzo hayo kupata umahiri wa kusimamia ,kuendesha na kuboresha huduma za afya kama inavyobainishwa kwenye mpango wa Tano wa sekta ya Afya.

"Mtumie Stadi mtakayopata za kuboresha wa huduma kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma bora yenye kiwango kulingana na viwango vilivyowekwa na serikali"

Awali Mkuu wa Taasisi  ya Cedha ,dkt Johannes Lukumay alisema serikali imewekeza kiasi cha zaidi ya sh, Trilioni 6.7 katika sekta ya Afya nchini na hivyo kuwataka wataalamu na viongozi wa sekta ya afya kutosita kujiendeleza kwa kuchukua mafunzo mbalimbali yanayotolewa na CEDHA na hivyo kuboresha huduma ya afya nchini. 

Alisema katika kipindi cha mwaka 2023/24 wizara ya Afya imeandaa mpango Mkakati wa kuboresha ubora wa huduma za afya kwa kutekeleza programu ya Mabadiliko ya kiutendaji kwa wasimamizi na watoa huduma za Afya ili kuongea uwajibikaji,ufanisi na tija katika utoaji wa huduma kwa ngazi zote.

Alisema ili kufikia malengo wizara kupitia Taasisi yake ya maendeleo ya Elimu ya watumishi wa Afya CEDHA, inatoa mafunzo ya muda mfupi kwa mujibu wa kalenda ya mwaka.

Dkt Lukumay alisema kuwa mafunzo hayo yenye washiriki takribani 30 yanajikita kwenye maulana Uongozi, Utawala na huduma Bora kwa vituo vya kutolea Huduma za Afya.









Ends.....





 








Post a Comment

0 Comments