Nq Joseph Ngilisho ARUSHA
Watu zaidi ya 20 wamefariki dunia katika ajali mbaya iliyotokea eneo la Kibaoni, Ngaramtoni ,wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha ikihusisha magari matatu kugongana.
Miongoni mwa watu waliofariki wamo raia 7 wa kigeni ,Hata hivyo majeruhi hadi sasa ni zaidi ya 20 ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa Mount meru na Hospital ya ALMC-Seliani
Chanzo cha ajali hiyo ni baada ya lori lenye tela lililokuwa limepakia mtambo wa kutengeneza barabara (Brudoza)kuacha njia baada ya kufeli breki na kuparamia magari matatu ambayo ni Coster ,Haice na gari binafsi lililokuwa imepakia raia wa kigeni ambao saba kati yao wanahofiwa kufariki dunia eneo la tukio .
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya Rufaa Mt Meru ,huku majeruhi wakipelekwa kupatiwa matibabu katika hospitali ya ALMC na Mount Meru jijini hapa.
Akitoa taarifa hiyo katika eneo la ajali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamshna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema ajali hiyo imetokea februari 24,2024 muda wa saa 11 jioni ambapo iliyohusisha lori na magari madogo matatu katika eneo la Ngaramtoni Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.
Kamanda Masejo amesema wanaendelea na uchunguzi wakina wa ajali hiyo ili kubaini chanzo halisi cha tukio.
Aidha amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya mount Meru kutambua miili ya waliofariki katika ajali hiyo.
Naye kamishna wa polisi Operesheni na Mafunzo,CP Awadhi Haji amesema watu 25 wamefariki dunia huku wengine 21 wakijeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea eneo la Kibaoni, Ngaramtoni by Pass ikihusisha Lori na magari mengine madogo matatu Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.
Akitoa taarifa hiyo baada ya kutembelea hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kulipolazwa majeruhi na miili ya marehemu.
Alisema ajali hiyo ilitokea Februari 24,2024 muda wa saa 11:00 jioni katika Barabara ya Arusha Namanga ambapo ilihusisha lori lenye namba za usajili KAC 943 H aina ya Mack lenye tela namba za usajili ZF 6778 mali ya kampuni ya KAY Construction ya Nairobi Nchini Kenya.
CP Awadhi ametaja idadi ya waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni wanaume (14) wanawake (10) na mtoto mmoja wa kike ambao jumla yao ni (25) huku akiitaja idadi ya raia 7 wa kigeni waliofariki .
Taarifa zaidi tutaendelea kuwajuza
0 Comments