(𝐈𝐦𝐞𝐚𝐧𝐝𝐢𝐤𝐰𝐚 𝐍𝐚 𝐏𝐚𝐮𝐥 𝐌𝐚𝐛𝐞𝐣𝐚)
BARAZA la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) limependekeza Rais kuondolewa mamlaka ya kuteua Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kutokuwapo kwa mgongano wa kimaslahi wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Mwenyekiti wa Tume ya Huduma za Kijamii wa Baraza hilo, Askofu Yuda Thadaeus Ruwa'ichi, alibainisha hayo jana alipowasilisha maoni ya TEC, kuhusu miswada minne ya sheria zinazohusu uchaguzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwenye Ukumbi wa Msekwa, bungeni jijini hapa.
Alisema TEC inapendekeza kuondolewa mamlaka ya Rais kuteua Mkurugenzi wa NEC kwa kuwa uteuzi huo kufanywa na Mkuu wa Nchi, kunaleta mgongano wa kimaslahi.
Ruwa'ichi ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, alisema wanapendekeza Mkurugenzi wa NEC ateuliwe na chombo huru badala ya utaratibu wa sasa wa Rais kuteua na kuwaapisha mwenyewe.
"Tunapendekeza Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kuteuliwa na chombo huru na kuapa kwa Jaji Mkuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani badala kuapa kwa Rais," alisema.
#NipasheMwangaWaJamii #NipasheHabari
0 Comments