TAZAMA UTAIPENDA, MFANYABIASHARA MONABAN ALIVYOSIMIKWA KUWA ASKOFU ,AWAKUMBUKA WAJUMBE CCM WALIVYOMLA KICHWA BAADA YA KUGOMBEA UBUNGE,MAPROFESA WAMSHAURI AACHANE NA SIASA ,MAMIA WAFURIKA KATIKA HEKALU LAKE JIPYA

Na Joseph Ngilisho ARUSHA 

Hatimaye Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM),limemsimika rasimi Mfanyabiashara na Mwanasiasa maarufu wa jiji Arusha Dkt Philemon Mollel (Monaban)kuwa askofu Mkuu Msaidizi wa kanisa hilo .


Awali mwaka juzi 2022,kanisa hilo lilimteua dkt Monaban na kumpa wadhifa huo wa kuliongoza kanisa hilo kabla ya kusimikwa rasimi jana.

Mei ,2022 Dkt Philemon Mollel alisimikwa kuwa Askofu, KKAM 

Askofu mkuu wa kanisa hilo, Oscar Ulotu alimsimika Dkt Mollel na kumwingiza kazini katika ibada iliyofurika mamia ya  watu wakiwemo viongozi wa dini mbalimbali ,Maprofesa na madaktari kutoka nchi mbalimbali viongozi wa serikali na wanasiasa.

Askofu Ulotu alitoa rai kwa viongozi wa dini hapa nchini kuwa wanyenyekevu na kuitii  serikali iliyopo madarakani hatua itakayosaidia kuondoa migogoro isiyo na tija.


Ibada hiyo ilifanyika katika kanisa hilo lililopo Ngulelo nje kidogo ya jiji la Arusha.


Askofu Ulotu alimpongeza dkt Mollel kwa kufikia daraja hilo la uaskofu na kusisitiza kuwa kiongozi bora lazima awe mnyenyekevu na mtii kwa watu wote ikiwemo anaowaongoza na asitumie nafasi hiyo kuwagandamiza kwa maslahi yake.


"Watumishi wengi wa mungu hawajafundishwa darasani unyenyekevu na utii ndio maana wengi wao wamekuwa wakipotosha na kukiuka sheria za nchi ,lazima tuitii serikali na kuisikiliza kwa sababu ndio yenye mamlaka"


Hata hivyo aliwataka viongozi hao kutoogopa kukemea maovu ili kuwarejesha kwenye mstari wanaoenda kinyume na maandiko matakatifu kwa sababu uwezo huo wanao .


Akiongea kwa niaba ya maprofesa na madaktari waliohudhulia hafla hiyo, Mwenyekiti wa umoja wa Maprofesa na Madaktari Tanzania(APDPT) Prof, Rejoke Ndalima alisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa chanzo cha migogoro ndani ya dini zao kuharibubkanisa  na hivyo kuhatarisha uvunjifu wa amani.

Alisema viongozi wa kiroho baadhi yao wameacha misingi ya kidini ambayo ndio wajibu wao na kuweka kando upendo,moyo wa huruma na unyenyekevu badala yake wameweka  mbele chuki na maslahi binafsi.


Prof Ndalima alimshauri Askofu Monaban kujiweka kando na siasa ili amtumikie mungu kwani siasa hazimfai na tayari ameonja adha ya wajumbe.

"Ukirudi kwenye siasa umeisha wajumbe wanakusubiri, malizia uzee wako madhabahuni"


"Viongozi wa dini acheni mizengwe kupenda madaraka muda ukiisha mwachie mwingine kwa upendo ,wengine wakiangushwa wanaondoka hata na mafaili na funguo za ofisi wakiwa wamejaa chuki ya kuondoka madarakani "


"Mfano mzuri ni kanisa Katoliki huwezi kukuta mambo yao yapo hadharani leo nachukua nafasi hii kuwapongeza wakatoliki kwa utaratibu wa kanisa lao lazima tuwaige ili migogoro yenu iishe"


Alisema viongozi wengi wa kiroho hawana uwezo wa kielimu ya darasani wametanguliza mbele uchu wa madaraka ,alimtaka askofu aliyesimikwa kwenda kupunguza migogoro makanisani.


Akishukuru baada ya kusimikwa, Askofu dkt Philemon Mollel,alisema wajibu uliombele yake ni kwenda kulitumikia kanisa kwa moyo wake wote huku akimtanguliza mungu na kuwashukuru wote waliofanikisha uteuzi wake.

Alisema amekuwa mtumishi wa kawaida kwa muda mrefu akilitumikia kanisa na watu mbalimbali hivyo kupata daraja hilo ni kusudi la mungu...


Alisema akiwa mtumishi wa mungu, mfanyabiashara na mwanasiasa alijifunza mengi na aliwahi kugombea ubunge jimbo la Arusha mjini lakini  aliona mengi ikiwemo wajumbe walivyomshughulikia kumwangusha ,hivyo ameona bora amtumikie mungu .


Alisema kwa sasa amepata wito wa kumtumikia mungu kama kiongozi mwenye wito na maono na atatumika wakati wowote na amejipanga kukemea maovu ili Tanzania liwe taifa la wacha mungu.


"Wakati wote wa kazi yangu nitakemea na kulaani matendo maovu yakiwemo haya yanayotikisa dunia ya kushabihikia mapenzi ya jinsia moja ,unyanyasaji wa wanawake na watoto ,sote tuungane kupaza sauti ,kanisa letu linapinga kwa nguvu zote  vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja ambavyo ni machukizo ya mungu"


Akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela,mwakilishi wa mkuu huyo ,Daniel Loiruck alisema serikali ya mkoa inatambua na kuthamini mchango wa kanisa hilo na taàsisi zote za dini.

Aliahidi kushirikiana na kanisa hilo katika kuijenga jamii ya watu wa Mkoa huo na tanzania kwa ujumla .


Alimpongeza askofu Mollel  kupata daraja la uaskofu na kumtakia afya njema katika utumishi wake uliotukuka huku akiwataka maaskofu wenzake kumpatia ushirikiano na miongozo ya kidini ili kuepusha migogoro  huku akitanguliza mbele maslahi ya kanisa na taifa kwa ujumla"Alisema .














                                      




Ends..













Post a Comment

0 Comments