Na Joseph Ngilisho ARUSHA
Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya ya Arusha, linawashikilia wafanyabiashara sita wa jijini hapa, wakituhumiwa kuuza sukari kwa bei ya juu kinyume na bei elekezi ya serikaki ya sh,3000.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa wilaya hiyo Felician Mtahengerwa alisema kuwa watu hao wamekamatwa katika kata tofauti kufuatia operesheni kali inayoendelea dhidi ya wafanyabiashara wanaoihujumu serikali kwa kuwaibia wananchi .
Alisema wafanyabiashara hao walikamatwa baada ya kukutwa wakiwauzia wananchi sukari kati ya sh,3200 hadi 4500 kinyume na bei elekezi ya serikali ya sh,3000 na
kudai kwamba wanakabiliwa na kosa la uhujumu uchumi ili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wengine wenye tamaa ya kujipatia kipato kikubwa kupitia changamoto ya sukari.
"Hawa wafanyabiashara wamekutwa wakiuza sukari zaidi ya bei elekezi ya serikali hii ni kinyume ya maelekezo ya waziri mwenye dhamana na bodi ya sukari nchini na hivuo kuwaumiza wananchi, tuliwaambia hatua mzaha juu ya hili na leo watakuwa mfano kwa wengine wenye tabia kama hiyo"
Mtahengerwa aliwataka wafanyabiashara wasioweza kufuata utaratibu na maelekezo ya serikali wasifanye biashara hiyo ya sukari katika wilaya yake.
"Kwa sababu ya kiburi cha wafanyabiashara sheria inakwenda kuchukua mkondo wake na nimemwagiza ocd afuate taratibu zote za kuwafikisha mahakamani kujibu shtaka lauhujumu uchumi"
Mkuu huyo amewaonya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaofanyabiashara hiyo kiujanja ujanja kwa kuingiza sukari kwa njia za panya na kuiuza kinyemela bila kufuata utaratibu kuwa watakamatwa muda wowote kwani wanafuatiliwa nyendo zao.
Ends...
0 Comments