TAZAMA JICHO LA ARUMERU MAGHARIBI LILIVYOCHACHU YA MAENDELEO, LIMEFANIKIWA KUWABANA VIONGOZI WASILALE ILI KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI

Na Joseph Ngilisho ARUMERU 

 Kikundi cha Maendeleo  cha  Arumeru Magharibi,Mkoani Arusha ,kinachojihusisha na uangalizi wa  viongozi waliochaguliwa na wananchi ,kimeeleza namna kilivyofanikiwa kuchochea mendeleo katika jimbo hilo kwa kuhakikisha viongozi waliochaguliwa na wananchi wanawajibika ipasavyo.

Akiongea katika Mkutano wao wa mwaka uliofanyika katika jimbo hilo,katika halmashauri ya Arusha,Mwenyekiti wa kikundi hicho,Abraham Singeen alisema kuwa kundi hilo lenye wanachama zaidi ya 400 liliundwa mahususi kama jicho la wanaarumeru Magharibi, kwa lengo la kuchochea maendeleo ili kuwaondolea changamoto wananchi.

Kundi hili ni jicho la wanaarumeru kama kuna changamoto sisi ndo tunawasukuma viongozi  ili wawajibike ipasavyo kuwahudumia wananchi,na hili tunalifanya  kwa nia njema na sio nia ya kudhalilishana ama kunyang'anyana madaraka" 

Alisema tangia kuundwa kwa kundi hilo mwaka 2021 ,mbali na kuwa jicho la wanaarumeru pia kundi hilo ambalo ni chachu ya maendeleo, limekuwa likijitolea vitu mbalimbali kwa jamii ikiwemo kuchangia fedha ,madawati kwa lengo la kutatua changamoto kwa wananchi.

"Tumekuwa tukifanya hivyo kwa lengo la kusaidia wanaarumeru Magharibi na wananchi wamekuwa wakileta kero kwetu na sisi tunazungumza na kiongozi wa eneo husika na tumefanikiwa kuwakumbusha majukumu yao na jamii inatupongeza sana "

Mwenyekiti huyo alisema mbali ya mafanikio hayo pia kundi hilo limeweza kuzalisha vikundi vingine vya kiuchumi kwa lengo kusaidiana na kuinuana kiuchumi.

Katika hatua nyingine wananchama wa kundi hilo walijadili mambo mbalimbali na miongoni mwa masuala hayo ni suala la mmomonyoka wa maadili, lilitiliwa mkazo ,huku jamii ya wamasai ikitakiwa kuzingatia malezi ya watoto wao ambao baadhi yao wameanz kukengeuka kwa kuacha mila na desturi za kabila hilo . 

Hoja jingine lililowasilishwa  katika mkutano huo ni suala la elimu  ambapo wanachama waliwashauri viongozi wa halmashauri hiyo kuangalia namna ya halmashauri hiyo kuwa na chuo kikuu walau kimoja ama chuo cha Ufundi VETA ili vijana wao wanaomaliza elimu ya msingi ama sekondari  waweze kujiendeleza kuliko kujiingiza kwenye makundi yasio faa.

Mwanachama wa kikundi hicho dkt Johannes Lukumay akizungumzia sekta ya afya alisema utafiti  wa kidunia ulivyofanywa mwaka 2019 inakadiliwa watu wapatao 860,000 walifariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya  ukimwi(VVU) na watu 640,000 walikufa kutokana na Malaria na watu 1,270,009 walikufa kutokana na usugu wa  dawa dhidi ya Vimelea.

Dkt Lukumay alisisitiza uwepo wa elimu zaidi kwa jamii kuhusu matumizi mabaya ya dawa ya antibiotics inayosababisha vifo.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha (Arusha DC)  Ojung'u Salekwa aliwataka wakazi wa jimbo hilo kuacha uvivu,wivu na majungu badala yake wachape kazi huku wakiipigania jamii yao kwa kujiletea maendeleo.

Aliwashauri wazazi kuwalea watoto wao katika misingi ya dini na kuwa na hofu  ya mungu na kutosahau mila na desturi zao .

Alisema amepokea baadhi ya hoja zilizosemwa na jicho la wanaarumeru Magharibi na kusema kuwa amezibeba na ataziwasilisha kama zilivyo  katika vikao vya halimashauri hiyo.


Miongoni mwa wanachama wa kundi hilo, ni pamoja na madiwani ,mbunge wenyeviti wazee wa ukoo,wafanyabiashara na wananchi mbalimbali. 










Ends...
















Post a Comment

0 Comments